46. Madhehebu ya Dhwaahiriyya kuhusu kupangusa juu ya soksi

6 – Madhehebu ya Dhwaahiriyyah:

Imaam Ibn Hazm (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu chake ”al-Muhallaa”:

”Kuweka sharti kwamba soksi ziwe na ngozi hakuna maana, kwa sababu haikuja katika Qur-aan, Sunnah, kipimo wala maneno ya Swahabah. Kuzuia kupaka juu ya soksi ni kosa, kwa sababu ni kinyume cha Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia kinyume cha masimulizi. Isitoshe Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakubagua soksi za ngozi kutokana na kitu kingine.”[1]

[1] al-Muhallaa (2/87).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 70
  • Imechapishwa: 20/04/2026