Imaam Ibn-ul-Qayyim amesema:
”Asiyelazimiana na Maandiko wakati mwingine huongeza katika Maandiko kile ambacho si miongoni mwake na husema kuwa ni kipimo. Mara nyingine hupunguza baadhi ya yanayolazimu ndani yake na kuitoa katika hukumu yake na husema kuwa huko ni kufanya umaalum. Mara nyingine huacha Maandiko kabisa na husema kuwa hayafanyiwi kazi au akasema kuwa hivo ni kinyume cha kipimo au kinyume cha misingi… Nasi tunaona kwamba kadiri mtu anavyozama zaidi katika kipimo, ndivyo anavyozidi kwenda kinyume na Sunnah. Hatuoni kupingwa kwa Sunnah na masimulizi isipokuwa kwa watu wa maono na kipimo. Ni Sunnah ngapi sahihi na zilizo wazi zimeachwa kwa sababu yake! Ni masimulizi mangapi zimepotea hukumu zake kwa sababu yake! Basi Sunnah na masimulizi kwa watu wa maono na watu wa kipimo ni tupu juu ya misingi yake, zimeachwa hukumu zake, zimeondolewa mamlaka na uongozi wake. Zina jina tu na hukumu ni ya vingine. Vinginevyo ni kwa nini iachwe Hadiyth ya kupaka juu ya soksi?”[1]
Kwa maana pamoja na kwamba imethibiti katika Sunnah, bali kipimo pia kinaithibitisha kama utakavyoona katika maneno ya Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).
[1] I´laam-ul-Muwaqqi´iyn (1/299).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 69-70
- Imechapishwa: 20/04/2026
Imaam Ibn-ul-Qayyim amesema:
”Asiyelazimiana na Maandiko wakati mwingine huongeza katika Maandiko kile ambacho si miongoni mwake na husema kuwa ni kipimo. Mara nyingine hupunguza baadhi ya yanayolazimu ndani yake na kuitoa katika hukumu yake na husema kuwa huko ni kufanya umaalum. Mara nyingine huacha Maandiko kabisa na husema kuwa hayafanyiwi kazi au akasema kuwa hivo ni kinyume cha kipimo au kinyume cha misingi… Nasi tunaona kwamba kadiri mtu anavyozama zaidi katika kipimo, ndivyo anavyozidi kwenda kinyume na Sunnah. Hatuoni kupingwa kwa Sunnah na masimulizi isipokuwa kwa watu wa maono na kipimo. Ni Sunnah ngapi sahihi na zilizo wazi zimeachwa kwa sababu yake! Ni masimulizi mangapi zimepotea hukumu zake kwa sababu yake! Basi Sunnah na masimulizi kwa watu wa maono na watu wa kipimo ni tupu juu ya misingi yake, zimeachwa hukumu zake, zimeondolewa mamlaka na uongozi wake. Zina jina tu na hukumu ni ya vingine. Vinginevyo ni kwa nini iachwe Hadiyth ya kupaka juu ya soksi?”[1]
Kwa maana pamoja na kwamba imethibiti katika Sunnah, bali kipimo pia kinaithibitisha kama utakavyoona katika maneno ya Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).
[1] I´laam-ul-Muwaqqi´iyn (1/299).
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 69-70
Imechapishwa: 20/04/2026
https://firqatunnajia.com/45-watu-pekee-wanaoipuuza-sunnah/