30 – Kutotekeleza haki za mume

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na na Shari´ah ni mwanamke kutotekeleza haki za mume. Baadhi ya wanawake – Allaah awaongoze – hawatimizi haki za waume zao kama inavyotakiwa. Hawazingatii haki zao na hawatii amri zao. Pengine pia anamdharau, anamtusi na kunyanyua sauti yake juu yake. Huenda vilevile akajizuilia nafsi yake pale anapomtaka, jambo ambalo halijuzu. Hivyo basi mche Allaah, ee mjakazi wa Allaah, na kuwa ni miongoni mwa wale wanaomfurahisha mume pale anapomtazama, anamtii pale anapomwamrisha na anajihifadhi nafsi yake na mali yake pale anapokuwa mbali naye.

Namuomba Allaah akusaidie kutekeleza yale uliyoelekezwa na akusaidie kuepuka yale uliyotahadharisha nayo, kwani hakika Yeye ndiye msaidizi bora na mnusuraji bora.

Swalah, amani na baraka zimwendee kiumbe wake mbora; Muhammad bin ´Abdillaah, jamaa zake na Maswahabah zake wote.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 36
  • Imechapishwa: 23/03/2026