45. Radd ya tatu juu ya makafiri wenye kupinga kufufuliwa


Isitoshe punje ya mbegu hii kavu Allaah anapoimwagilia maji ikachipua mimea na ikakuwa mpaka mwishowe ikazalisha mashuke na matunda ilihali hapo kabla ilikuwa ni punje ya mbegu kavu ambayo Allaah amezalisha mmea huu wa kushangaza:

أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ

“Je, huyo hakuwa ni muweza wa kuhuisha wafu?”[1]

Tone la manii ni kama mbegu. Tone la manii yanachanganyikana manii ya mwanaume na manii ya mwanamke, kisha yanageuka kuwa pande la damu, kisha damu hiyo inakuwa kinofu cha nyama, kisha kinofu cha nyama kinakuwa viungo vya mwili, mishipa, akasikia, akaona, akahisi, kisha akapuliziwa roho halafu akapewa uhai:

أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ

“Kwani hakuwa tone linalotokana na manii yanayomwagwa kwa nguvu, kisha akawa pande la damu, akamuumba na akamsawazisha, akamfanya pea mbili; mwanamme na mwanamke? Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kuwahuisha wafu?”[2]

Yule ambaye ameweza kugeuza tone hili la manii kutoka katika maji yaliyochanganyikana kutoka katika manii ya mwanaume na manii ya mwanamke na kuwa mtu. Huyu ambaye amemuumba mtu huyu kutoka katika manii haya na akamkuza ni muweza juu ya kumuisha baada ya kufa kwake. Ikiwa wanasema kwamba anapotea na kumalizika ndani ya ardhi basi Allaah (Jalla wa ´Alaa) anasema:

قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ

“Hakika Sisi tunajua kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao [miili yao iliyokufa] na tunacho Kitabu kinachohifadhi.”[3]

Udongo unaombadilisha mtu huyu utamrudisha kuwa damu na viungo kama alivyokuwa kabla. Mabaki haya yatarudishwa na kuwa kama yalivyokuwa hapo kabla na hakutopotea kitu. Hata kama atateketea yeye wote na kuwa udongo kuna kitu ambacho hakiteketei ambacho ni kiungo kidogo kiitwacho عجب الذنب  “kifupa kilicho kwenye uti wa mgongo wa mtu”. Kiungo hichi hakiteketei. Kutoka kwenye kiungo hichi ndio hutengenezwa uumbaji wa mtu.

[1] 75:40

[2] 75:37-40

[3] 50:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 07/04/2021