Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Aidha wanadhani kwamba wale waliokuja nyuma waliyafahamu maandiko yaliyofasiriwa kwa majaaz na maneno ye kigeni. Dhana hii mbovu ndio imepelekea katika maneno kama hayo ambayo yamefanya Uislamu ukatupiliwa mbali. Wameusemea uongo mfumo wa Salaf na wakapotea kwa kuupa kipaumbele mfumo wa waliokuja nyuma. Matokeo yake wamekusanya kati ya kujahili mfumo wa Salaf kwa kule kuwasemea uongo na ujinga na upotevu kwa kule kuupa kipaumbele mfumo wa wale waliokuja nyuma.

MAELEZO

Wale waliokuja nyuma wanayageuza maandiko kutoka nje ya maana yake sahihi. Wanazingatia hiyo ndio elimu na tafsiri sahihi. Kuona kuwa elimu ya wale waliokuja nyuma ni bora kuliko elimu ya Salaf ni njia fulani ya kuutupilia mbali Uislamu. Wanawasemea uwongo Salaf pale wanapowatuhumu ujinga na kwamba walikuwa wakiamini maandishi pasi na kuelewa maana yake. Sambamba na hilo wamepotea pindi wanaposifu mfumo wa wale waliokuja nyuma ambao ni kule kuyapindisha maandiko kutokana na maana yake sahihi. Kwa hivyo wakakusanyika kati ya kuwasemea uwongo Salaf na upotofu pale wanapofadhilisha mfumo wa wale waliokuja nyuma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 79
  • Imechapishwa: 07/08/2024