Ni jambo linaloruhusu kwa mfungaji kujipoza kwa maji kwa kuoga mwili wake wote, lakini ajihadhari maji yasiingie kooni.
Mwenye kula au kunywa kwa kusahau basi hana kosa juu yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwenye kusahau hali ya kuwa amefunga ambapo akala na kunywa, basi akamilishe swawm yake. Hakika si vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[1]
Hili ni miongoni mwa upole wa Allaah kwa waja Wake na kuwarahisishia. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… akamilishe swawm yake.”
ni dalili ya wazi kwamba funga yake ni sahihi.
Vivyo hivyo ikiwa vumbi au nzi vitaingia kooni mwake, hilo halina athari juu ya swawm yake kwa saabu ya kutowezekana kuepuka jambo hilo.
Tambueni ya kwamba – Allaah akurehemu – ya kwamba ni wajibu kwa muislamu kuilinda funga yake dhidi ya mambo yanayoiharibu au yanayopunguza thawabu yake. Ikiwa jambo lolote katika hayo litatokea kwa njia ya kusahau, basi hana dhambi juu yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ummah wake umesamehewa makosa yanayotokana na kukosea, kusahau na kulazimishwa.”[2]
[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).
[2] at-Twabaraaniy (02/97) (nr. 1430) kwa tamko lisemalo:
”Allaah ameusamehe ummah wangu mambo matatu.”
Ni yenye kutoka kwa Thawbaan.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 43
- Imechapishwa: 16/03/2026
Ni jambo linaloruhusu kwa mfungaji kujipoza kwa maji kwa kuoga mwili wake wote, lakini ajihadhari maji yasiingie kooni.
Mwenye kula au kunywa kwa kusahau basi hana kosa juu yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwenye kusahau hali ya kuwa amefunga ambapo akala na kunywa, basi akamilishe swawm yake. Hakika si vyenginevyo Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[1]
Hili ni miongoni mwa upole wa Allaah kwa waja Wake na kuwarahisishia. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… akamilishe swawm yake.”
ni dalili ya wazi kwamba funga yake ni sahihi.
Vivyo hivyo ikiwa vumbi au nzi vitaingia kooni mwake, hilo halina athari juu ya swawm yake kwa saabu ya kutowezekana kuepuka jambo hilo.
Tambueni ya kwamba – Allaah akurehemu – ya kwamba ni wajibu kwa muislamu kuilinda funga yake dhidi ya mambo yanayoiharibu au yanayopunguza thawabu yake. Ikiwa jambo lolote katika hayo litatokea kwa njia ya kusahau, basi hana dhambi juu yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ummah wake umesamehewa makosa yanayotokana na kukosea, kusahau na kulazimishwa.”[2]
[1] al-Bukhaariy (1933) na Muslim (1155).
[2] at-Twabaraaniy (02/97) (nr. 1430) kwa tamko lisemalo:
”Allaah ameusamehe ummah wangu mambo matatu.”
Ni yenye kutoka kwa Thawbaan.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 43
Imechapishwa: 16/03/2026
https://firqatunnajia.com/45-mfungaji-kujipoza-kwa-maji-na-vumbi-au-nzi-kumuingia-kooni/