Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Niacheni muda wa kuwa nimekuacheni. Hakika hapana vyenginevyo kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuuliza kwao kwa wingi na kutofautiana kwao na Mitume wao. Ninapokukatazeni jambo basi liepukeni na ninapokuamrisheni lifanyeni muwezavyo.”[1]
Shaykh na ́Allaamah ́Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy amesema wakati alipokuwa akitoa maelezo ya Hadiyth hiyo:
“Miongoni mwa yanayoingia katika Hadiyth hii ni kuuliza namna zilivyo sifa za Muumba. Sifa zote zinatakiwa kukabiliwa kama alivyosema Imaam Maalik wakati alipoulizwa kuhusu namna ya Kulingana juu ya ´Arshi:
“Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Kwa hivyo mtu akiuliza ni vipi ujuzi wa Allaah au namna ya uumbaji na kuyaendesha Kwake mambo, basi ataambiwa kama ambavyo dhati ya Allaah haifanan na dhati za viumbe basi kadhalika sifa za Allaah hazifanani na sifa Zake. Viumbe wanamjua Allaah na zile sifa na matendo Yake aliyowajuza. Kuhusu namna zilivyo sifa Zake hakuna yeyote anayejua hilo isipokuwa Allaah pekee.”[2]
Yaliyotangulia juu ni baadhi ya mambo yanayotilia nguvu juu ya masimulizi ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah):
”Kulingana juu si kitu kisichojulikana. Namna haifahamiki. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo..”
Makusudio haya ni kuashiria tu baadhi ya yale yenye kuitia nguvu. Vinginevyo kupambanua kwa kina ni jambo litarefusha sana.
[1] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
[2] Bahjat Quluub-il-Abraar, uk. 219.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 66-67
- Imechapishwa: 05/12/2025
Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Niacheni muda wa kuwa nimekuacheni. Hakika hapana vyenginevyo kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuuliza kwao kwa wingi na kutofautiana kwao na Mitume wao. Ninapokukatazeni jambo basi liepukeni na ninapokuamrisheni lifanyeni muwezavyo.”[1]
Shaykh na ́Allaamah ́Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy amesema wakati alipokuwa akitoa maelezo ya Hadiyth hiyo:
“Miongoni mwa yanayoingia katika Hadiyth hii ni kuuliza namna zilivyo sifa za Muumba. Sifa zote zinatakiwa kukabiliwa kama alivyosema Imaam Maalik wakati alipoulizwa kuhusu namna ya Kulingana juu ya ´Arshi:
“Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Kwa hivyo mtu akiuliza ni vipi ujuzi wa Allaah au namna ya uumbaji na kuyaendesha Kwake mambo, basi ataambiwa kama ambavyo dhati ya Allaah haifanan na dhati za viumbe basi kadhalika sifa za Allaah hazifanani na sifa Zake. Viumbe wanamjua Allaah na zile sifa na matendo Yake aliyowajuza. Kuhusu namna zilivyo sifa Zake hakuna yeyote anayejua hilo isipokuwa Allaah pekee.”[2]
Yaliyotangulia juu ni baadhi ya mambo yanayotilia nguvu juu ya masimulizi ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah):
”Kulingana juu si kitu kisichojulikana. Namna haifahamiki. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo..”
Makusudio haya ni kuashiria tu baadhi ya yale yenye kuitia nguvu. Vinginevyo kupambanua kwa kina ni jambo litarefusha sana.
[1] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
[2] Bahjat Quluub-il-Abraar, uk. 219.
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 66-67
Imechapishwa: 05/12/2025
https://firqatunnajia.com/45-mfano-wa-maswali-yaliyokatazwa/