128 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Shaytwaan anamjilia mmoja wenu na kusema “Ni nani kaumba kadhaa, ni nani kaumba kadhaa” mpaka anamwambia “Ni nani kamuumba Mola wako?”” Anapomfikisha huko basi aombe kinga kwa Allaah na akomeke.”[1]
MAELEZO
Katika Hadiyth hii imekuja ya kwamba anapoingiwa na wasiwasi basi ni lazima kwake afanye mambo haya mawili:
1 – Amwombe Allaah (´Azza wa Jall) kinga kutokana na shaytwaan.
2 – Akomeke. Kwa maana aache kufikiri na ajishughulishe na jambo jengine.
Imekuja katika Hadiyth nyenginezo ya kwamba ambaye atafikwa na wasiwasi katika Tawhiyd basi afanye mambo kadhaa yanayochukuliwa katika mkusanyiko wa maandiko. Nayo ni mambo sita:
Mambo mawili yametajwa katika Hadiyth hii. Nayo ni yafuatayo:

2 – Akomeke. Kwa maana aache kufikiri na ajishughulishe na haja zake zingine.
Kuhusu mambo mengine ni kama yafuatayo:
3 – Apulize upande wake wa kushoto mara tatu[2].
4 – Asome Suurah “al-Ikhlaasw”[3].
5 – Asome:
هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ٌ
“Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho na Aliye juu na Aliye karibu – Naye juu ya kila jambo ni mjuzi.”[4][5]
6 – Aseme:
“Nimemwamini Allaah na Mtume Wake.”[6]
Mtu akifanya mambo yote haya basi Allaah (Ta´ala) anamsalimisha kutokana na wasiwasi.
[1] al-Bukhaariy (3276) na Muslim (134).
[2] Abu Daawuud (4722).
[3] Abu Daawuud (4722).
[4] Abu Daawuud (5110).
[5] 57:03
[6] al-Bukhaariy (3055) na Muslim (134).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 122-123
- Imechapishwa: 10/11/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 122-123
Imechapishwa: 10/11/2025
https://firqatunnajia.com/45-duaa-unapopatwa-na-wasiwasi/