45. Damu kwa ajili ya kipimo au kumpa mgonjwa mwingine kwa mfungaji

Swali 45: Kuchotwa damu kwa lengo la kufanyiwa kipimo au kujitolea kumpa mwingine mchana wa Ramadhaan kunamfunguza mfungaji?

Jibu: Mtu akichotwa damu kidogo isiyomuathiri akawa dhaifu mwilini mwake hafungui kwa jambo hilo. Ni mamoja amechotwa kwa ajili ya kipimo, kuchunguza maradhi fulani au kujitolea kumpa mtu mwingine anayehitajia. Lakini akichotwa damu kiwango kikubwa kinachofanya mwili kudhoofika basi anafungua kwa kitendo hicho kwa kulinganisha (قياسا) na kufanyiwa chuku ambako kumethibiti katika Sunnah kwamba kunamfunguza mfungaji.

Kujengea juu ya hayo haijuzu kwa mtu kujitolea kiwango hicho cha damu ilihali amefunga swawm ya lazima kama mfano wa funga ya Ramadhaan. Isipokuwa kama kuna dharurah. Katika hali hiyo ajitolee damu hiyo kwa ajili ya kukidhi dharurah hiyo na hivyo anakuwa amefungua ambapo atatakiwa kula na kunywa siku yake iliobaki na atalipa badala ya siku hiyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 39
  • Imechapishwa: 01/05/2021