Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

74 – Imani ni kukubali kwa ulimi na kusadikisha kwa moyo.

MAELEZO

Hii ni ´Aqiydah ya Hanafiyyah na Maaturiydiyyah, tofauti na ´Aqiydah ya Salaf na kikosi kikubwa cha  maimamu, akiwemo Maalik, ash-Shaafi´iy, Ahmad na al-Awzaa´iy. Bali na kukubali na kusadikisha, hawa wengine wameongeza matendo ya viungo vya mwili.

Makinzano kati ya ´Aqiydah hizo mbili sio ya kisura kabisa, kama alivosema mshereheshaji (Rahimahu Allaah), kwa kutumia hoja kwamba wote wameafikiana juu ya kwamba mtenda dhambi kubwa hatoki nje ya imani na kwamba yuko chini ya utashi wa Allaah kwa njia ya kwamba akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu. Hebu wacha tuseme kuwa maafikiano hayo ni sahihi; endapo Hanafiyyah wasingekuwa wametofautiana na kikosi kikubwa cha wanazuoni makinzano ya kihakika na wakapinga kuwa matendo ni katika imani, basi wangeliungana na kikosi na kusema kwamba imani inazidi kwa matendo mema na kushuka kwa maasi, jambo ambalo kuna dalili nyingi juu yake katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf juu yake. Mshereheshaji amenakili kundi kubwa zuri katika wao. Hata hivyo Hanafiyyah wameamua kuendelea kushikia msimamo wao na kutofautiana na dalili zinazotamka wazi juu ya kupanda na kushuka. Badala yake wakajikakama katika kuyafasiri kujikamama kwa wazi na kuliko batili. Mshereheshaji ametaja baadhi ya tafsiri hizo. Bali amemnukuu Abul-Mu´iyn an-Nasafiy ambaye ameponda usahihi wa Hadiyth ”Imani ni tanzu sabini na kitu… ”licha ya kuwa maimamu wote katika Hadiyth, akiwemo al-Bukhaariy na Muslim wameijengea hoja[1] katika ”as-Swahiyh” zao, kwa sababu Hadiyth ni dalili ya waziwazi dhidi ya ´Aqiydah yao.

Ni vipi makinzano yatakuwa ya kisura peke yake ilihali wanaona kuwa inafaa kwa mtenda dhambi kusema kuwa imani yake ni kama ya imani ya Abu Bakr as-Swiddiyq, imani ya Mitume na Manabii na imani ya Jibriyl na Mikaaiyl (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam)? Itakuweje, ilihali wao kutokana na ´Aqiydah yao, hawamjuzishii yeyote, pasi na kujali namna atakavyokuwa mtenda dhambi, kusema kuwa ni muumini – Allaah akitaka? Wao wanaona kuwa ni lazima kwake kusema kuwa ni muumini wa kweli. Ilihali Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا

“Hakika si venginevyo waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zaozinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea; ambao wanasimamisha swalah na hutoa sehemu katika yale tuliyowaruzuku – hao ndio waumini wa kweli!”[2]

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

“… na nani mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?”[3]

Kisha ushabiki wao ukaenda mbali zaidi. Wanasema kuwa yule mwenye kufanya uvuaji katika imani yake ni kafiri. Kutokana na hilo wakasema kuwa haijuzu kwa ambaye ni katika Hanafiyyah kumuoa mwanamke ambaye ni katika Shaafi´iyyah. Baadhi yao wengine wakaonyesha ”kuvumiliana” na wakasema kuwa inafaa lakini si kinyume chake. Hoja yao ni kwamba mwanamke wa Shaafi´iyyah ana hukumu moja kama hukumu ya wanawake wa Kitabu! Mimi namjua Shaykh mmoja wa Hanafiyyah ambaye alimposa msichana wake kwa Shaykh mmoja wa Shaafi´iyyah. Lakini baba akakataa posa hiyo kwa sababu ni katika Shaafi´iyyah. Je, baada ya haya mtu anaweza kutilia shaka ya kwamba makinzano ni ya kihakika? Yule anayetaka kubobea katika mada hii basi arejee ”Kitaab-ul-Iymaan” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, kwani ni kitabu bora juu ya maudhui haya.

[1] Nimeitaja Hadiyth hiyo katika ”as-Swahiyhah” (1769).

[2] 08:02-04

[3] 4:122

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 66-69
  • Imechapishwa: 02/10/2024