4 – Amesema kuwa kuuliza juu yake ni Bid´ah. Kwa sababu kuuliza na kupekua jambo hilo ni jambo ambalo hakuliamrisha kwa waja. Bali maandiko yanafahamisha kuwa ni jambo lisilowezekana na kwamba hakuna njia ya kulitambua. Kwa ajili hiyo yule mwenye kulipekua na akatafiti kulijua atazungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
”Je, mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?”[1]
Kitendo hicho ni miongoni mwa madhambi makubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
”Sema: “Hakika si vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyo ya siri na dhambi ukandamizaji bila ya haki na kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo hakukiteremshia dalili na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui”.”[2]
Mwenye kufanya hivo ametamka pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ
“Na wala usiyafuate yale usiyokuwa nayo elimu.”[3]
Isitoshe, kutokana na akili yake pungufu, amemtangulia mbele Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Enyi walioamini! Msitangulie mbele ya Allaah na Mtume Wake na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote!”[4]
Jengine ni kwamba Qur-aan na Sunnah vimekataza kuuliza juu ya vitu vilivyojificha, yale mambo ambayo Allaah ameyasamehe kwa namna ya kwamba hakuyawajibisha wala kuyaharamisha pamoja na makatazo ya kuuliza maswali ya kujikakama na kuhojihoji. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ
“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.”[5]
[1] 2:80
[2] 7:33
[3] 17:36
[4] 49:1
[5] 5:101
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 66
- Imechapishwa: 05/12/2025
4 – Amesema kuwa kuuliza juu yake ni Bid´ah. Kwa sababu kuuliza na kupekua jambo hilo ni jambo ambalo hakuliamrisha kwa waja. Bali maandiko yanafahamisha kuwa ni jambo lisilowezekana na kwamba hakuna njia ya kulitambua. Kwa ajili hiyo yule mwenye kulipekua na akatafiti kulijua atazungumza juu ya Allaah pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
”Je, mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?”[1]
Kitendo hicho ni miongoni mwa madhambi makubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
”Sema: “Hakika si vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyo ya siri na dhambi ukandamizaji bila ya haki na kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo hakukiteremshia dalili na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui”.”[2]
Mwenye kufanya hivo ametamka pasi na elimu. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ
“Na wala usiyafuate yale usiyokuwa nayo elimu.”[3]
Isitoshe, kutokana na akili yake pungufu, amemtangulia mbele Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Enyi walioamini! Msitangulie mbele ya Allaah na Mtume Wake na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote!”[4]
Jengine ni kwamba Qur-aan na Sunnah vimekataza kuuliza juu ya vitu vilivyojificha, yale mambo ambayo Allaah ameyasamehe kwa namna ya kwamba hakuyawajibisha wala kuyaharamisha pamoja na makatazo ya kuuliza maswali ya kujikakama na kuhojihoji. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ
“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.”[5]
[1] 2:80
[2] 7:33
[3] 17:36
[4] 49:1
[5] 5:101
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 66
Imechapishwa: 05/12/2025
https://firqatunnajia.com/44-ni-bidah-kuuliza-juu-ya-kulingana-juu/