Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Hivyo, ikiwa atakubali ya kwamba makafiri wanashuhudia kuwa uola wote ni wa Allaah, na kwamba hawakutaka chochote kutoka kwao zaidi isipokuwa uombezi, lakini anachotaka ni kutofautisha baina ya kitendo chao na kitendo chake kwa kile alichokitaja, mkumbushe ya kwamba [miongoni mwa] makafiri kulikuwa wanaoabudu watu wema na masanamu, na miongoni mwao kulikuwa wanaowaomba mawalii. Ambao Allaah anasema juu yao:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta njia ya kwenda kwa Mola – na hata miongoni mwa waliokaribu mno.” (17:57)
Na wanamuomba ´Iysaa bin Maryam na mama yake. Allaah amesema:
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
“al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote isipokuwa ni Mtume tu; bila shaka wamekwishapita kabla yake Mitume wengine, na mama yake ni mkweli – wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayah kisha tazama vipi wanavyogeuzwa.” (05:75)
MAELEZO
Bi maana mtu huyo akijua kuwa washirikina walikuwa wakithibitisha uola na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mola, muumbaji na mmiliki wa kila kitu na kwamba waliabudu masanamu haya ili tu yapate kuwakurubisha mbele ya Allaah na wawaombee, amekubali hilo na kwamba makusudio yao wao na makusudio yake ni mamoja. Pamoja na hivyo ´Aqiydah yao haikuwanufaisha chochote.
Mtunzi (Rahimahu Allaah) amsema:
“… mkumbushe ya kwamba… “
Hili ni jibu la “Hivyo ikiwa atakubali… “. Mkumbushe kuwa kuna washirikina ambao walikuwa wakiyaomba masanamu kwa ajili ya kutaka uombezi, kama ambavyo pia ndio lengo lako pia. Pia kulikuwa washirikina wanaoabudu mawalii, kama unavyofanya wewe na hivyo mna lengo na mungu mmoja. Dalili ya kwamba wanawaomba mawalii ni maneno Yake (Ta´ala):
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta njia ya kwenda kwa Mola – na hata miongoni mwa waliokaribu mno.”
Vilevile kulikuwa wenye kuwaabudu Mitume, kama ambavyo manaswara wanavyofanya kwa kumuabudu al-Masiyh bin Maryam, na wengine walikuwa wakiwaabudu Malaika. Amesema (Ta´ala):
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ
“Na Siku Atakayowakusanya wote kisha atawaambia Malaika: “Je, hawa ndio waliokuwa wakikuabuduni?”” (34:40)
Jibu hili linafichua udanganyifu wake ya kuwa washirikina wanaabudu masanamu na yeye anawaabudu mawalii na Mitume, kwa njia mbili:
1 – Uanganyifu wake si sahihi kwa kuwa kuliwepo pia washirikina wenye kuabudu mawalii na waja wema.
2 – Lau tutakadiria kuwa walikuwa wakiabudu masanamu peke yake, hakuna tofauti kati yake yeye na wao. Kwa sababu wote ni waja wasioweza kumnufaisha yeyote kwa chochote.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 62
- Imechapishwa: 12/11/2023
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Hivyo, ikiwa atakubali ya kwamba makafiri wanashuhudia kuwa uola wote ni wa Allaah, na kwamba hawakutaka chochote kutoka kwao zaidi isipokuwa uombezi, lakini anachotaka ni kutofautisha baina ya kitendo chao na kitendo chake kwa kile alichokitaja, mkumbushe ya kwamba [miongoni mwa] makafiri kulikuwa wanaoabudu watu wema na masanamu, na miongoni mwao kulikuwa wanaowaomba mawalii. Ambao Allaah anasema juu yao:
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta njia ya kwenda kwa Mola – na hata miongoni mwa waliokaribu mno.” (17:57)
Na wanamuomba ´Iysaa bin Maryam na mama yake. Allaah amesema:
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
“al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote isipokuwa ni Mtume tu; bila shaka wamekwishapita kabla yake Mitume wengine, na mama yake ni mkweli – wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayah kisha tazama vipi wanavyogeuzwa.” (05:75)
MAELEZO
Bi maana mtu huyo akijua kuwa washirikina walikuwa wakithibitisha uola na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Mola, muumbaji na mmiliki wa kila kitu na kwamba waliabudu masanamu haya ili tu yapate kuwakurubisha mbele ya Allaah na wawaombee, amekubali hilo na kwamba makusudio yao wao na makusudio yake ni mamoja. Pamoja na hivyo ´Aqiydah yao haikuwanufaisha chochote.
Mtunzi (Rahimahu Allaah) amsema:
“… mkumbushe ya kwamba… ”
Hili ni jibu la “Hivyo ikiwa atakubali… “. Mkumbushe kuwa kuna washirikina ambao walikuwa wakiyaomba masanamu kwa ajili ya kutaka uombezi, kama ambavyo pia ndio lengo lako pia. Pia kulikuwa washirikina wanaoabudu mawalii, kama unavyofanya wewe na hivyo mna lengo na mungu mmoja. Dalili ya kwamba wanawaomba mawalii ni maneno Yake (Ta´ala):
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ
“Hao wanaowaomba [wao wenyewe] wanatafuta njia ya kwenda kwa Mola – na hata miongoni mwa waliokaribu mno.”
Vilevile kulikuwa wenye kuwaabudu Mitume, kama ambavyo manaswara wanavyofanya kwa kumuabudu al-Masiyh bin Maryam, na wengine walikuwa wakiwaabudu Malaika. Amesema (Ta´ala):
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ
“Na Siku Atakayowakusanya wote kisha atawaambia Malaika: “Je, hawa ndio waliokuwa wakikuabuduni?”” (34:40)
Jibu hili linafichua udanganyifu wake ya kuwa washirikina wanaabudu masanamu na yeye anawaabudu mawalii na Mitume, kwa njia mbili:
1 – Uanganyifu wake si sahihi kwa kuwa kuliwepo pia washirikina wenye kuabudu mawalii na waja wema.
2 – Lau tutakadiria kuwa walikuwa wakiabudu masanamu peke yake, hakuna tofauti kati yake yeye na wao. Kwa sababu wote ni waja wasioweza kumnufaisha yeyote kwa chochote.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 62
Imechapishwa: 12/11/2023
https://firqatunnajia.com/44-mlango-wa-07-wenye-kuwaomba-uombezi-masanamu-na-maiti-lengo-lao-ni-moja/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)