28 – Kuhifadhi picha za baadhi ya wachezaji na wasanii

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na na Shari´ah ni yale yanayofanywa na baadhi ya wasichana katika kuhifadhi picha picha za baadhi ya wachezaji na wasanii na kubadilishana picha hizo kati ya wasichana. Hili linasababisha ukiukwaji wa Kishari´ah, ikiwa ni pamoja na moyo wa msichana huyo unakuwa umefungamana na picha hiyo. Hili ni jambo la khatari sana. Msichana huyo anashughulishwa kupenda picha hiyo badala ya kumpenda Mola wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Tunamuoba Allaah usalama na afya.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 22/03/2026