Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Hakika wazushi hawa wanafadhilisha mfumo wa waliokuja nyuma wa wanafalsafa kwa sababu wanadhani kwamba mfumo wa Salaf una maana ya kuamini tu maandiko ya Qur-aan na Sunnah bila kuyafahamu. Kwa msemo mwingine ni kama wale ambao si wasomi ambao Allaah amesema juu yao:
وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ
“Miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika, hawakijui Kitabu isipokuwa tu matamanio ya kuwaza tu, nao hawana isipokuwa kudhania tu.”[1]
MAELEZO
Dhana yao mbovu inatokana na msingi wao mbovu ambao ni kuwatuhumu Salaf ujinga na sambamba na hilo kuwasifu wale waliokuja nyuma. Je, ni kweli Salaf wako namna hiyo? Sivyo kabisa. Salaf walikuwa wakiamini matamshi na maana, wanayaamini na wanayafasiri kwa njia sahihi.
Wanafalsafa wanaokusudiwa ni wanafalsafa wa kigiriki ambao wale waliokuja nyuma wakachukua ´Aqiydah kutoka kwao na wakaitendea kazi. Je, hawa wanaweza kulinganishwa na Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy na Maswahabah wengine waliosalia? Je, hawa wanaweza kulinganishwa na wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah, zile karne bora? Wanafalsafa hawana jengine isipokuwa tu elimu ya falsafa, elimu ya mantiki na elimu ya mijadala ambayo imetoka kwa wanafalsafa wa kigiriki. Salaf wameichukua elimu yao kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walijifunza Qur-aan na Sunnah. Ni vipi mtu ambaye ni bingwa wa Qur-aan na Sunnah anaweza kulinganishwa na mtu ambaye amebobea katika elimu ya mantiki, mijadala na theolojia ambayo imetoka kwa wanafalsafa wa kigiriki makafiri ambao hawana utambuzi juu ya Shari´ah?
Watu hawa wamedhani kuwa Salaf walikuwa si wasomi na wamefanana na mayahudi ambao Allaah amesema juu yao:

“Miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika, hawakijui Kitabu isipokuwa tu matamanio ya kuwaza tu, nao hawana isipokuwa kudhania tu.”
Bi maana kundi la watu ambao wanasoma bila kufahamu maana. Miongoni mwa watu wa Kitabu ipo sampuli ya watu hawa.
Shaykh (Rahimahu Allaah) anabainisha sababu iliyowafanya watu hawa kuwafadhilisha wale waliokuja nyuma juu ya Salaf; wamefikiri kuwa wale waliokuja nyuma wameyajua mambo ambayo hayakujulikana kwa Salaf. Wakimaanisha kuwa Salaf walikuwa tu wakisoma Qur-aan pasi na kuifahamu tofauti na wale waliokuja nyuma ambao wameelewa tafsiri na maana yake. Isitoshe ni kina nani hawa Salaf wanaokusudiwa? Na ni kina nani hawa waliokuja nyuma wanaokusudiwa? Salaf ni wale Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah. Hawa ndio karne bora inapokuja katika elimu, matendo na ´Aqiydah. Ummah unachukua elimu na dini kutoka kwao, kwa sababu wao ndio wakati na kati baina ya ummah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu wale waliokuja nyuma wanaosimangwa, wanakusudiwa wasomi wa wanafalsafa, wasomi wa theolojia na wasomi wa mantiki ambao wameichukua elimu yao kutoka kwa wanafalsafa. Je, hivi kweli hawa wanaweza kulinganishwa na wale wengine? Ambaye amechukua elimu yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutoka kwa Maswahabah anaweza kulinganishwa na ambaye ameichukua elimu yake kutoka kwa wanafalsafa na wasomi wa kigiriki wa mantiki ambayo hakuna kheri wala faida yoyote ndani yake? Huko mbele mtakuja kuona jinsi walivyojutia wale wakuu wao kutokana na mfumo wao huu.
[1] 02:78
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 77-78
- Imechapishwa: 06/08/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 77-78
Imechapishwa: 06/08/2024
https://firqatunnajia.com/44-hakuna-awezaye-kulinganishwa-na-salaf/