192 – Hishaam bin Khaalid ametukhabarisha: al-Waliyd bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Lahiy´ah, kutoka kwa ´Uqayl, kutoka kwa az-Zuhriy: ´Abdul-Malik bin Abiy Bakr bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Dharr, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Qiyaamah hakitosimama mpaka mpumbavu, mwana wa mpumbavu, aitawale dunia. Mbora wa watu kipindi hicho ni muumini baina ya wazazi watukufu wawili.”[1]
193 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: Ibraahiym bin Sa´d ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin Abiy Bakr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Swahabah mmoja wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kunakaribia mpumbavu, mwana wa mpumbavu, kuitawala dunia.”
194 – Muhammad bin ´Awf ametukhabarisha: Abul-Yamaan ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´ayb, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin Abiy Bakr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Swahabah mmoja wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wa hayo.
195 – ´Umar bin al-Khattwaab ametukhabarisha: ´Amr bin ´Uthmaan ametukhabarisha: Aswbagh bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa Ja´far bin Burqaan, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab: Nimemsikia ´Umar bin al-Khattwaab akielezea kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Miongoni mwa alama za Qiyaamah ni aitawale dunia mpumbavu, mwana wa mpumbavu. Mbora wa watu ni muumini baina ya wazazi watukufu wawili.”
196 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, kutoka kwa ´Abdullaah bin Abdir-Rahmaan al-Ashhaliy, kutoka kwa Hudhayfah, ambaye ameeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Qiyaamah hakitosimama mpaka mwenye furaha zaidi ulimwenguni awe ni mpumbavu, mwana wa mpumbavu.”[2]
197 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ja´far bin ´Awn na al-Fudhwayl bin Dukayn wametukhabarisha, kutoka kwa al-Waliyd bin Jamiy´: Abu Bakr bin Abiyl-Jahm ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Niyaar – mmoja katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Dunia haitomalizika mpaka iwe kwa mpumbavu, mwana wa mpumbavu.”[3]
[1] at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” (3076). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (1505).
[2] at-Tirmidhiy (2209). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2209).
[3] Nzuri kwa mujibu wa as-Suyuutwiy katika “al-Jaamiy´ as-Swaghiyr (9747).
- Muhusika: : Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 49-51
- Imechapishwa: 14/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket