197 – ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Mu-addil ametukhabarisha: Aliy al-Husayn bin Swafwaan al-Bardha´iy ametuzindua: ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Ishaaq bin Mansuur ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Sulaymaan, kutoka kwa ´Amr bin Maalik, kutoka kwa Abul-Jawzaa’, aliyesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا

”Na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka.”[1]

”Bi maana kuyaahirisha mambo.”

198 – Ibn Abiyd-Dunyaa amesema: Sa´d bin Zunbuur al-Hamdaaniy ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuzindua, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Abu Ishaaq, aliyesema:

”Bwana mmoja katika ´Abdul-Qays aliombwa kutoa nasaha, ambapo akasema: ”Jihadhari na ´nita´.”

199 – Ibraahiym bin ´Umar al-Barmakiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Khalaf ad-Daqqaaq ametuzindua: Muhammad bin Swaalih bin Dhariyh ametuhadithia: Hannaad bin as-Sarriy ametuhadithia: Ibn-ul-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Waarith, kutoka kwa bwana mmoja, kutoka kwa al-Hasan, aliyesema:

”Jihadhari na kuyaahirisha mambo. Unaishi hivi sasa na si kesho. Ukikutana na kesho basi ishi kesho hiyo kama ulivyoishi siku ya leo, na usipokutana na kesho basi hutojutia juu ya uliyoyakosa leo.”

200 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ismaa´iyl al-Haashimiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Ubayd ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ibraahiym amenihadithia: Swaalih al-Murriy ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Abul-Jald, aliyesema:

”Nilisoma kwenye kitabu kimoja ´Nita` ni askari miongoni mwa maaskari wa Ibliys.”

201 – Muhammad bin Ahmad bin Rizquuyah na ´Aliy bin Ahmad bin ´Umar al-Muqriy wametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad al-Khuldiy ametukhabarisha: Ibraahiym bin Naswr al-Mansuuriy ametuhadithia: Ibraahiym bin Bashshaar amenihadithia: Yuusuf bin Asbaatw amenihadithia: Muhammad bin Samurah as-Swaa-ih aliniandikia ujumbe ufuatao:

”Ndugu yangu kipenzi! Jihadhari kwa sababu kuahirisha kunaufunga moyo wako. Kunapelekea katika unyonge na uharibifu, kunazima matumaini na kukata muda wa kueshi. Ukifanya hivo, basi utaweka badala yake azma yako ambapo inafelisha vitendo vyako juu yake na inakurudishia uchovu ambao hapo awali ulikuondokea. Ikirudi kwako, basi kamwe nafsi yako haitonufaika chochote na mwili wako. Fanya haraka, ee ndugu kipenzi, kwani unafanywa haraka! Fanya haraka, kwani unaharakishwa! Harakisha, kwani unaharakishwa! Kuwa mwenye kumaanisha kweli, basi jambo ni kubwa. Amka kutoka usinginzini mwako na zindukana kwenye kupumbaa kwako. Kumbuka yale yaliyokupita, ukayafanyia upungufu, ukazembea, ukakiuka na kufanya. Yote hayo yameandikwa na kudhibitiwa. Unaonekana uko katika hali ambayo imekushangaza na ambapo unafurahiya ulichokifanya na kujutia ulichokosea.”

Mwisho

Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah pekee. Swalah na amani zimwendee Muhammad na kizazi chake.

[1] 18:28

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 27/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy