Kisha Shaykh (Rahimahu Allaah) akafasiri al-Faatihah kwa kifupi hali ya kusema:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”[1]
Baraka na kuomba msaada.
MAELEZO
Maana yake ni kwamba muislamu anatakiwa kuleta Basmalah kwa ajili kutafuta baraka kwa jina la Allaah na kuomba msaada kutoka kwa Allaah katika kisomo chake. Na hali ni hiyo pia katika kila jambo analolitangulia kwa kutaja jina la Allaah – analitaja kwa ajili ya kutafuta baraka na msaada wa Allaah. Asome Basmalah kimyakimya.
Je, Basmalah ni Aayah ndani ya Qur-aan na Aayah mwanzoni mwa kila Suurah. Kwa maana ya kwamba ni Aayah yenye kujitegemea kwa ajili ya kutenganisha baina ya Suurah na ni Aayah ya sehemu ya Suurah ”al-Faatihah” au siyo? Wanazuoni wana mitazamo tofauti juu ya hayo. Dalili kuwa ni sehemu ya Qur-aan ni kwamba Maswahabah waliingiza ndani ya msahafu na hawakuandika isipokuwa ambacho ni Qur-aan tu. Imekuja katika ”Sunan Abiy Daawuud” kwa mlolongo wa wapokezi (788) kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza ya kwamba:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akijua mwisho wa Suurah hadi anapoteremshiwa:
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”
[1] 01:01
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 50-51
- Imechapishwa: 02/06/2026
Kisha Shaykh (Rahimahu Allaah) akafasiri al-Faatihah kwa kifupi hali ya kusema:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”[1]
Baraka na kuomba msaada.
MAELEZO
Maana yake ni kwamba muislamu anatakiwa kuleta Basmalah kwa ajili kutafuta baraka kwa jina la Allaah na kuomba msaada kutoka kwa Allaah katika kisomo chake. Na hali ni hiyo pia katika kila jambo analolitangulia kwa kutaja jina la Allaah – analitaja kwa ajili ya kutafuta baraka na msaada wa Allaah. Asome Basmalah kimyakimya.
Je, Basmalah ni Aayah ndani ya Qur-aan na Aayah mwanzoni mwa kila Suurah. Kwa maana ya kwamba ni Aayah yenye kujitegemea kwa ajili ya kutenganisha baina ya Suurah na ni Aayah ya sehemu ya Suurah ”al-Faatihah” au siyo? Wanazuoni wana mitazamo tofauti juu ya hayo. Dalili kuwa ni sehemu ya Qur-aan ni kwamba Maswahabah waliingiza ndani ya msahafu na hawakuandika isipokuwa ambacho ni Qur-aan tu. Imekuja katika ”Sunan Abiy Daawuud” kwa mlolongo wa wapokezi (788) kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza ya kwamba:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akijua mwisho wa Suurah hadi anapoteremshiwa:
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”
[1] 01:01
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 50-51
Imechapishwa: 02/06/2026
https://firqatunnajia.com/43-mitazamo-tofauti-ya-wanazuoni-kuhusu-basmalah/