Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri – zikimtazama Mola wake.”[1]
Wafasiri wa Qur-aan, kama vile Ibn ´Abbaas, Muhammad bin Ka´b, ´Abdur-Rahmaan bin Saabit, al-Hasan bin Abiyl-Hasan, ´Ikrimah, Abu Swaalih, Sa´iyd bin Jubayr na wengineo katika Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah, wameafikiana kwamba watatazama uso wa Mola wao. Kuna wengine wametoa maana kama hiyo. Wale waliopokea kwamba watasubiri malipo ni maoni dhaifu ambayo hayakuthibiti. Hapa uso wa Allaah (´Azza wa Jall) unaweza kufasiriwa kwa njia mbili: uso wa kweli na malipo.
Kuhusu yale yenye maana ya uso wa kweli, ni yale yaliyopokelewa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Muusa, Swuhayb na wengineo. Vivyo vivyo zile Hadiyth ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaomba kwa uso Wake (´Azza wa Jall), akajilinda na uso wa Allaah, akaomba kutazama uso wa Allaah, akakataza kuomba kwa uso wa Allaah, akasema kuwa uso wa Allaah ni nuru inayoangazia nuru ya mbingu na kwamba Allaah (´Azza wa Jall) anapowaridhia watu fulani, basi huwaelekea kwa uso Wake. Hali kadhalika maneno Yake (´Azza wa Jall):

“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri – zikimtazama Mola wake.”
Kwa mujibu wa maana ya maimamu ni kutazama uso wa Allaah wa kikweli; ahadi ambayo Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamewaahidi mawalii wa Allaah. Waliwapa bishara njema waumini ya kutazama uso wa Allaah (´Azza wa Jall).
Kuhusu yale yenye maana ya thawabu ni maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا
“Hakika si vyenginevyo sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutafuta uso wa Allaah, hatukusudii kwenu malipo na wala shukurani.”[2]
Vivyo hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimzungumzia mzungumzaji anayejibidisha kutafuta uso wa Allaah na Hadiyth mfano wa hizo. Hizo zinakusudia thawabu.
Tawfiyq ni yenye kutoka kwa Allaah. Himdi zote njema anastahiki Allaah.
[1] 75:22-23
[2] 76:9
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 101
- Imechapishwa: 20/10/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri – zikimtazama Mola wake.”[1]
Wafasiri wa Qur-aan, kama vile Ibn ´Abbaas, Muhammad bin Ka´b, ´Abdur-Rahmaan bin Saabit, al-Hasan bin Abiyl-Hasan, ´Ikrimah, Abu Swaalih, Sa´iyd bin Jubayr na wengineo katika Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah, wameafikiana kwamba watatazama uso wa Mola wao. Kuna wengine wametoa maana kama hiyo. Wale waliopokea kwamba watasubiri malipo ni maoni dhaifu ambayo hayakuthibiti. Hapa uso wa Allaah (´Azza wa Jall) unaweza kufasiriwa kwa njia mbili: uso wa kweli na malipo.
Kuhusu yale yenye maana ya uso wa kweli, ni yale yaliyopokelewa katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Muusa, Swuhayb na wengineo. Vivyo vivyo zile Hadiyth ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaomba kwa uso Wake (´Azza wa Jall), akajilinda na uso wa Allaah, akaomba kutazama uso wa Allaah, akakataza kuomba kwa uso wa Allaah, akasema kuwa uso wa Allaah ni nuru inayoangazia nuru ya mbingu na kwamba Allaah (´Azza wa Jall) anapowaridhia watu fulani, basi huwaelekea kwa uso Wake. Hali kadhalika maneno Yake (´Azza wa Jall):
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri – zikimtazama Mola wake.”
Kwa mujibu wa maana ya maimamu ni kutazama uso wa Allaah wa kikweli; ahadi ambayo Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamewaahidi mawalii wa Allaah. Waliwapa bishara njema waumini ya kutazama uso wa Allaah (´Azza wa Jall).
Kuhusu yale yenye maana ya thawabu ni maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا
“Hakika si vyenginevyo sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutafuta uso wa Allaah, hatukusudii kwenu malipo na wala shukurani.”[2]
Vivyo hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimzungumzia mzungumzaji anayejibidisha kutafuta uso wa Allaah na Hadiyth mfano wa hizo. Hizo zinakusudia thawabu.
Tawfiyq ni yenye kutoka kwa Allaah. Himdi zote njema anastahiki Allaah.
[1] 75:22-23
[2] 76:9
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 101
Imechapishwa: 20/10/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/43-mara-uso-mara-thawabu/