27 – Maovu katika sherehe za ndoa

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na na Shari´ah ni yale yanayofanyika kwenye sherehe za ndoa ikiwa ni pamoja na israfu katika mavazi, kusikiliza nyimbo zisizo na maadili kwenye kanda, kucheza kwa mdundo wa kanda hiyo isiyo na maadili, mambo ambayo hayafai. Kilichothibiti kwa mujibu wa Sunnah ni kupiga dufu ambayo imefunikwa ngozi upande mmoja tu. Vivyo hivyo yanaingia pia yale yanayofanyika katika kuchukua picha au kurekodi video na pia matumizi ya vipaza sauti vinavyosababisha sauti za wanawake kufika nje, mambo ambayo hayajuzu.

Kwa hivyo, dada yangu wa Kiislamu, jihadhari kutokana na mambo hayo. Ukialikwa kwenye ndoa na ukajua ya kwamba kutakuwa na maovu na wakati huohuo unaweza kuyazuia basi hudhuria na uyazuie. Vinginevyo ni haramu kwako kwenda katika harusi hiyo.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 35
  • Imechapishwa: 22/03/2026