Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hatumshuhudii muislamu yeyote kwa kitendo alichofanya kuingia Peponi wala Motoni. Tunatarajia kwake mema na tunachelea kwake. Tunachelea kwa mtenda dhambi na tunatarajia kwake huruma ya Allaah.”
MAELEZO
Haifai kumshuhudia muislamu yeyote kwamba ataingia Peponi wala Motoni, kwa sababu hatujui ni kipi Allaah atafanya kwa waja Wake. Lakini hata hivyo tunamkufurisha mtu ambaye amekufuru mpaka akawa ni murtadi. Ama ambaye ni muislamu na amefanya madhambi makubwa yasiyomtoa katika Uislamu, jambo lake liko kwa Allaah; akitaka atamsamehe, na akitaka atamuadhibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninaapa kwa Allaah kwamba mimi ni Mtume wa Allaah na sijui ni yepi yatayopitika na mimi.”[1]
Kwa hayo sisi tuna haki zaidi ya kutomshuhudilia yeyote kuingia Peponi. Isipokuwa yule ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam amemshuhudilia kwamba ataingia Peponi, kama wale kumi walioshuhudiliwa Pepo, Thaabit bin Qays bin Shimmaas na mwanamke yule aliyekuwa na ugonjwa kifafa (Radhiya Allaahu ´anhum). Katika hali haii na sisi tunatakiwa kuwashuhudilia Pepo. Ama kuhusu wengine, sisi tunatarajia kheri na Pepo kwa wale waja wema na wakati huohuo tunachelea juu ya wale watenda madhambi na tunaliacha jambo lao kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] al-Bukhaariy (3929).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 151-152
- Imechapishwa: 02/05/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)