Vivyo hivyo kuhusiana na Hadiyth:

”Allaah hufurahishwa zaidi na tawbah ya mja wake zaidi kuliko vile anavyofurahi mmoja wenu pale anapomkosa ngamia wake ambaye yuko na chakula na kinywaji chake juu yake. Kisha akamtafuta na asimpate. Baada ya hapo akalala chini ya mti na huku akisubiria kifo. Tahamaki ngamia yule amesimama juu yake. Akamshika khatamu na kwa furaha nyingi akasema: ”Ee Allaah! Wewe ni mja wangu na mimi ndiye Mola Wako.”

Furaha ya Allaah ni sifa ya Allaah inayolingana Naye. Anafurahi lakini hata hivyo sio kama wanavyofurahi viumbe. Anaridhia lakini lakini sio kama wanavyoridhia viumbe. Anakasirika lakini lakini sio kama wanavyokasirika viumbe. Hadiyth hii inahusiana na mtu aliyempoteza ngamia wake na alikuwa jangwani amelala chini ya mti na huku anasubiri tu mauti yamfike. Tahamaki akamuona ngamia wake amesimama juu ya kichwa chake. Akasema kutokana na wingi wa furaha:

”Ee Allaah! Wewe ni mja wangu na mimi ndiye Mola Wako.”

Alikosea kutokana na wingi wa furaha. Allaah (Subhaanah) ni mwenye furaha zaidi juu ya tawbah ya mja Wake kuliko mtu huyu. Pamoja na kuwa Yeye ndiye ambaye amemtunukia tawbah hii. Lakini pamoja na hivyo anaifurahikia kutoka kwa mja Wake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ndiye ambaye amemtunukia na kumjaalia kufanya hivo. Tunamuomba Allaah atusamehe sote.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 60
  • Imechapishwa: 23/10/2024