2- Tawassul iliyokatazwa: Ni kutawassul kwa Allaah kwa jaha ya mtu, kwa haki ya mtu kwa Allaah au kwa dhati ya mtu. Hii ni Tawassul iliyokatazwa na ni njia miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki. Kwa hiyo ni wajibu kutofautisha baina ya tTwassul inayojuzu na Tawassul iliyokatazwa.

Shaykh Taqiyy-ud-Diyn Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu “at-Tawassul wal-Wasiylah” ya kwamba kumetokea makosa katika mlango huu kwa sababu ya kuchanganya na kutatiza mambo. Kwa hiyo ni wajibu kutambua Tawassul zinazojuzu na Tawassul zilizokatazwa ili mtu asiingie katika makosa. Huu ni mlango mkubwa. Ni wajibu kuyatilia umuhimu ili mambo yasichanganyike au shubuha za watu hawa wapotofu zikawatatiza baadhi ya watu na wale wasiokuwa wasomi. Ni wajibu kujua majibu juu yake ili mambo yasichanganyike.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 69
  • Imechapishwa: 02/09/2018