126 – al-Baraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Tulikuwa tunaposwali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tunapenda kuwa upande wake wa kulia na yeye anatuelekea kwa uso wake. Tukamsikia akisema:

رَبِّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ – أَوْ تَجمَعُ – عِبَادَكَ

 “Mola nikinge na adhabu siku utayofufua – au akikusanya – waja Wako.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii imekuja ya kwamba du´aa hii imewekwa katika Shari´ah baada ya kumaliza kuswali:

رَبِّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ – أَوْ تَجمَعُ – عِبَادَكَ

 “Mola nikinge na adhabu siku utayofufua – au akikusanya – waja Wako.”

Vilevile imesuniwa kuisoma wakati wa kulala, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anataka kulala, huweka mkono wake chini ya kichwa chake kisha anasema:

رَبِّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ – أَوْ تَجمَعُ – عِبَادَكَ

 “Mola nikinge na adhabu siku utayofufua – au akikusanya – waja Wako.”[2]

[1] Muslim (709).

[2] Sunan-it-Tirmidhiy (3398).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 119-120
  • Imechapishwa: 09/11/2025