Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

”Luutw alipowaambia watu wake: “Je, mnafanya machafu ambayo hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?” Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Bali nyinyi ni watu wapindukiaji mipaka.” (07:80-81)

Hawa watu walipelekewa Nabii Luutw akawaonye kwa mabaya yao na awafundishe mema, walikuwa wakikaa Falastin (Palestine) na miji iliyokuwa karibu na hapo. Watu hao walikuwa wameharibika kweli kweli katika akhlaki (tabia) zao. Hao ndio watu wa mwanzo kuzua machafu ya wanaume kuwaingilia wanaume wenzao. Wakawa hawana haja ya wanawake kabisa. Basi Allaah akawapelekea Nabii Luutw – ambaye ni mtoto wa ami yake Nabii Ibraahiym na mfuasi wake Nabii Ibraahiym wa mwanzo. Alikuwa mfuasi wake tangu Nabii Ibraahiym alipokuwa ´Iraaq hata akenda Misri hata akaja Shaam. Kote alikuwa pamoja naye wakilingania watu kheri.

Na katika maasi yaliyokamatana na tupu hapana yaliyowekewa adhabu kubwa zaidi kuliko haya[1], kwa taathira yake mbaya.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/adhabu-ya-mashoga-katika-uislamu/

  • Mhusika: Shaykh ´Abdullaah Swaalih al-Farsiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurani Takatifu, uk. 196-197
  • Imechapishwa: 06/11/2018