Kitu pekee ambacho ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf au Sa´d bin Abiy Waqqaas alichokuwa anaomba anapokuwa akitufu katika Nyumba ya Allaah ilikuwa kusema:
“Mola wangu! Niepushe na uchoyo wa nafsi yangu! Mola wangu, niepushe na uchoyo wa nafsi yangu!” Akaambiwa: “Huwa huombi du´aa nyingine zaidi ya hii?” Akasema: “Nikiepushwa na uchoyo wa nafsi yangu basi hakika nimefaulu.”[1]
Tofauti kati ya uchoyo na ubakhili ni kwamba uchoyo ni pupa kali juu ya kitu, tamaa isiyoisha ya kukipata na kung’ang’ania kukusanya. Ni tamaa ya ndani ya nafsi kwa uchu wa kumiliki. Ama ubakhili ni kuzuia matumizi ya kile mtu alichokipata, kukipenda mno na kukihifadhi bila kukitoa. Hivyo mtu huwa mchoyo kabla hajakipata na huwa mbakhili baada ya kukipata. Ubakhili ni tunda la uchoyo na uchoyo ndio unaompeleka mtu kuwa mbakhili. Uchoyo unajificha ndani ya nafsi; anayekuwa mbakhili anakuwa ameitii nafsi yake ya uchoyo na asiye kuwa mbakhili anakuwa ameiasi nafsi yake ya uchoyo na ameepushwa na shari yake na huyo ndiye aliyefaulu:
وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
”Yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”[2]
[1] Jaamiy´-ul-Bayaan (23/286) ya ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf.
[2] 59:9 na 64:16
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 73
- Imechapishwa: 11/08/2025
Kitu pekee ambacho ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf au Sa´d bin Abiy Waqqaas alichokuwa anaomba anapokuwa akitufu katika Nyumba ya Allaah ilikuwa kusema:
“Mola wangu! Niepushe na uchoyo wa nafsi yangu! Mola wangu, niepushe na uchoyo wa nafsi yangu!” Akaambiwa: “Huwa huombi du´aa nyingine zaidi ya hii?” Akasema: “Nikiepushwa na uchoyo wa nafsi yangu basi hakika nimefaulu.”[1]
Tofauti kati ya uchoyo na ubakhili ni kwamba uchoyo ni pupa kali juu ya kitu, tamaa isiyoisha ya kukipata na kung’ang’ania kukusanya. Ni tamaa ya ndani ya nafsi kwa uchu wa kumiliki. Ama ubakhili ni kuzuia matumizi ya kile mtu alichokipata, kukipenda mno na kukihifadhi bila kukitoa. Hivyo mtu huwa mchoyo kabla hajakipata na huwa mbakhili baada ya kukipata. Ubakhili ni tunda la uchoyo na uchoyo ndio unaompeleka mtu kuwa mbakhili. Uchoyo unajificha ndani ya nafsi; anayekuwa mbakhili anakuwa ameitii nafsi yake ya uchoyo na asiye kuwa mbakhili anakuwa ameiasi nafsi yake ya uchoyo na ameepushwa na shari yake na huyo ndiye aliyefaulu:
وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
”Yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”[2]
[1] Jaamiy´-ul-Bayaan (23/286) ya ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf.
[2] 59:9 na 64:16
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 73
Imechapishwa: 11/08/2025
https://firqatunnajia.com/42-tofauti-kati-ya-uchoyo-na-ubakhili/