Ikiwa mwenye janaba au mwenye hedhi hakupata maji, basi afanye Tayammum na hapo itaruhusu kwake kusoma Qur-aan, kuswali na mengineyo. Ikiwa atapata hadathi, basi swalah itakuwa haramu kwake. Haisemi kuwa ni haramu kusoma Qur-aan wala kukaa msikitini na mengineyo ambayo hayaharamishwi kwa mwenye hadathi, kama vile kama angeoga kisha akapata hadathi. Hili ni katika mambo yanayoulizwa na kushangaza ambapo watu wanauliza itakuweje mtu mwenye janaba anazuiwa na swalah lakini hazuiwi kusoma Qur-aan, kukaa msikitini bila dharurah na mengineyo. Hivyo ndivyo ilivyo.
Kisha la kushangaza zaidi ni kwamba hakuna tofauti katika tuliyoyataja kati ya Tayammum ya mwenye janaba akiwa katika mji wake au safarini. Baadhi ya wafuasi wa ash-Shaafi´iy wametaja kwamba ikiwa atafanya Tayammum akiwa katika mji wake, basi anarusiwa kuswali lakini asisome Qur-aan baada yake wala asikae msikitini. Maoni sahihi zaidi ni kujuzu kwa hayo, kama tulivyotangulia.
Lau atafanya Tayammum kisha akaswali na kusoma Qur-aan, kisha baadaye akaona maji ambayo ni lazima ayatumie, basi inakuwa haramu kwake kusoma na kila kinachoharamishwa kwa mwenye janaba mpaka pale atakapooga.
Endapo atafanya Tayammum, akaswali na kusoma Qur-aan, kisha akataka kufanya Tayammum kwa sababu ya hadathi, kwa ajili ya swalah nyingine ya faradhi au kwa sababu nyingine, basi haisemi kuwa ni haramu kwake kusoma kwa mujibu wa maoni sahihi na yaliyochaguliwa. Shaafi´iyyah wanayo maoni mengine yanayosema kuwa kitendo hicho hakijuzu, lakini maoni yanayotambulika ni yale ya kwanza.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 50-51
- Imechapishwa: 30/08/2026
Ikiwa mwenye janaba au mwenye hedhi hakupata maji, basi afanye Tayammum na hapo itaruhusu kwake kusoma Qur-aan, kuswali na mengineyo. Ikiwa atapata hadathi, basi swalah itakuwa haramu kwake. Haisemi kuwa ni haramu kusoma Qur-aan wala kukaa msikitini na mengineyo ambayo hayaharamishwi kwa mwenye hadathi, kama vile kama angeoga kisha akapata hadathi. Hili ni katika mambo yanayoulizwa na kushangaza ambapo watu wanauliza itakuweje mtu mwenye janaba anazuiwa na swalah lakini hazuiwi kusoma Qur-aan, kukaa msikitini bila dharurah na mengineyo. Hivyo ndivyo ilivyo.
Kisha la kushangaza zaidi ni kwamba hakuna tofauti katika tuliyoyataja kati ya Tayammum ya mwenye janaba akiwa katika mji wake au safarini. Baadhi ya wafuasi wa ash-Shaafi´iy wametaja kwamba ikiwa atafanya Tayammum akiwa katika mji wake, basi anarusiwa kuswali lakini asisome Qur-aan baada yake wala asikae msikitini. Maoni sahihi zaidi ni kujuzu kwa hayo, kama tulivyotangulia.
Lau atafanya Tayammum kisha akaswali na kusoma Qur-aan, kisha baadaye akaona maji ambayo ni lazima ayatumie, basi inakuwa haramu kwake kusoma na kila kinachoharamishwa kwa mwenye janaba mpaka pale atakapooga.
Endapo atafanya Tayammum, akaswali na kusoma Qur-aan, kisha akataka kufanya Tayammum kwa sababu ya hadathi, kwa ajili ya swalah nyingine ya faradhi au kwa sababu nyingine, basi haisemi kuwa ni haramu kwake kusoma kwa mujibu wa maoni sahihi na yaliyochaguliwa. Shaafi´iyyah wanayo maoni mengine yanayosema kuwa kitendo hicho hakijuzu, lakini maoni yanayotambulika ni yale ya kwanza.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 50-51
Imechapishwa: 30/08/2026
https://firqatunnajia.com/42-tayammum-kwa-ajili-ya-kusoma-qur-aan/