Tafiti ya tatu inahusu muda wa upangusaji. Jambo hili wanazuoni wametofautiana:

Kikosi cha walio wengi kati Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na wale waliokuja baada yao wanaona kuwa muda aliopangiwa ambaye ni mkazi ni mchana mmoja na usiku wake na michana mitatu na nyusiku zake kwa ambaye ni msafiri.

Wanazuoni wengine wanasema kuwa ufutaji ni kitu kisichokuwa na muda kabisa. Imekuja katika kitabu “al-Majmuu´”:

“Wenzetu wamenukuu maoni hayo kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan, ash-Sha´biy, Rabiy´ah, al-Layth na wengi katika wafuasi wa Maalik. Pia ndio maoni yaliyotangaa kwake. Ana maoni mengine yanayosema kuwa upangusaji umewekewa muda maalum. Ana maoni ya tatu yanayosema kuwa muda wa upangusaji amewekewa mkazi pasi na msafiri. Ibn-ul-Mundhir amesema:

“Sa´iyd bin Jubayr amesema: “Apanguse kunzia asubuhi mpaka usiku.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Upangusaji wa msafiri ambaye ana ugumu wa kuzivua na kuzivaa haukuwekewa muda maalum. Mfano wa mtu kama huyo ni mfanya kazi wa posta ambaye anafanya kazi kwa manufaa ya waislamu.”[2]

Muda huu unaanza kuhesabiwa kuanzia lini?

Wanazuoni wengi wanaona kuwa muda wa kupangusa unaanza kuhesabiwa kuanzia uchengukaji wa wudhuu´ wa kwanza baada ya kuzivaa. Imekuja katika “al-Majmuu´”:

“al-Awzaa´iy na Abu Thawr wamesema kuwa muda wa kupangusa unaanza kuhesabiwa tokea pale atakapoanza kupangusa baada ya kuchengukwa na wudhuu´. Haya ni maoni pia yaliyopokelewa kutoka kwa Ahmad na Daawuud. Ndio maoni ya dalili yenye nguvu. Yamechaguliwa na Ibn-ul-Mundhir na amenukuu mfano wake kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh). al-Maawardiy na ash-Shaashiy wamemnukuu al-Hasan al-Baswriy ambaye ameeleza kuwa muda wa kupangusa unaanza kuanzia pale kitapovaliwa kile kinachofunika mguu.”[3]

[1] al-Madmuu´ (1/467).
[2] al-Ikhtiyaaraat, uk. 15.
[3] al-Majmuu´ (1/470).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/185-186)
  • Imechapishwa: 11/05/2021