Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Haitoacha Jahannam kutupwa ndani yake [watu na mawe] nayo inasema:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Je, kuna zaidi?” (50:30)

mpaka Mola Mtukufu (Tabaarak wa Ta´ala) aweke Mguu Wake – na imekuja katika upokezi mwingine “unyayo Wake” juu yakwe kisha pawe sawa. Hapo ndio itasema ­­“Inatosha! Inatosha!”

“Haitoacha Jahannam kutupwa ndani yake [watu na mawe] nayo inasema “Je, kuna zaidi?”, mpaka al-Jabbaar aweke ndani yake Mguu Wake.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… Mguu Wake kisha pawe sawa. Hapo ndio itasema ­­“Inatosha! Inatosha!”[7]

Hapa Allaah anathibitishiwa kuwa na mguu na unyayo. Inatakiwa kuthibitisha mguu kwa njia inayolingana na Allaah. Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, ana mkono na mguu. Zote hizi ni sifa zinazolingana Naye. Hashabihiani na viumbe katika sifa Zake. Hafanani nao katika usikizi Wake, uoni Wake, mkono Wake, mguu Wake, kucheka Kwake na nyenginezo. Kucheka kwa Allaah na kusikia Kwake kunalingana Naye pekee na upande mwingine sifa za viumbe zinalingana nao. Amesema (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ

”Basi msipigie mifano Allaah!” (16:74)

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanasema namna hii kuhusu sifa zote. Mlango wake ni mmoja. Hili ni tofauti na Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah na wengineo waliozipotosha sifa za Allaah. Jahmiyyah wanakanusha majina na sifa za Allaah vyote viwili.

Mu´tazilah wanakanusha sifa na wakati huohuo wamethibitisha majina matupu yasiyokuwa na maana.

Ashaa´irah na mapote mengine wamekanusha baadhi ya sifa na wakati huohuo wakathibitisha sifa nyenginezo.

Sahihi ni kuthibitisha majina na sifa zote za Allaah zilizokuja katika Qur-aan na Sunnah. Yale yote yaliyosihi kupokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kama mfano wa yale yaliyokuja ndani ya Qur-aan. Ni wajibu kumthibitishia nayo Allaah kwa njia inayolingana Naye bila ya kupotosha, kukanusha, kuzifanyia namna na kulinganisha. Inatakiwa kuyathibitisha kwa mujibu wa maneno Yake (Subhaanah):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.”

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ

”Basi msipigie mifano Allaah!”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 23/10/2024