42. Je, kuzidishwe idadi ya Takbiyr maiti akiwa na ubora?

Swali 42: Je, kuzidishwe idadi ya Takbiyr maiti akiwa na ubora[1]?

Jibu: Bora ni kufupika na nne, kama inavofanywa hivi sasa. Kwa sababu hili ndilo la mwisho katika matendo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na an-Najaashiy licha ya kwamba anayo sifa kubwa ya kipekee. Alitosheka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kumpigia Takbiyr nne.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/148).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 34
  • Imechapishwa: 20/12/2021