42. Hivi ndivo kilianza kila kitu

41 – ´Imraan bin Huswayn amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Zipokeeni khabari njema, ee Banuu Tamiym!” Wakasema: ”Umetubashiria, hivyo tupe basi!” Akasema: ”Zipokeeni khabari njema, enyi watu wa Yemen!” Wakasema: ”Umetubashiria, basi hebu tueleze jambo zima lilianzaje!” Akasema: ”Allaah alikuwa juu ya ´Arshi na alikuwa kabla ya kila kitu. Akaandika kwenye Ubao kila kitu kitachokuwa.”

Hadiyth hii ni Swahiyh na ameipokea al-Bukhaariy katika maeneo mbalimbali[1].

[1] Hapa mtunzi (Rahimahu Allaah) anasema kuwa Hadiyth ni Swahiyh na kwamba ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” hii. Ingawa mara nyingi huashiria juu ya kusihi kwake kwa kuiegemeza kwa al-Bukhaariy na Muslim au mmoja wao. Kitendo cha imamu huyu kinafahamisha kufaa kufanya yote mawili, jambo ambalo mimi mwenyewe limelifanya katika baadhi ya kaguzi zangu. Hata hivyo likatuhumiwa na baadhi ya mashabiki wa Hanafiyyah kwa jambo ambalo hata sijawahi kulifikiria. Nimelifafanua hilo na nikaliraddi vilivyo katika utangulizi wa ukaguzi wangu wa chapa ya nne ya “Sharh al-´Aqiyah at-Twahaawiyyah”. Rejea huko, kwani ni jambo muhimu.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 98-99
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy