192 – Ibraahiym amesema: Ahmad bin ´Abdillaah bin Yuunus ametuhadithia: Nimemsikia Abu Bakr bin ´Ayyaash akimtaja Ajlah, ambaye amesema: adh-Dhwahhaak bin Muzaahim amesema:
”Fanya matendo kabla ya kutoweza kufanya matendo. Natamani ningeweza kufanya matendo leo, lakini siwezi.”
193 – Abu ´Abdillaah al-Husayn bin al-Hasan bin Ahmad bin Muhammad al-Jawaaliyqiy ametukhabarisha: Ja´far al-Khuldiy ametuhadithia: Ahmad – yaani Ibn Muhammad bin Masruuq – ametuhadithia: Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Muhammad bin Ashkaab ametuhadithia: Bwana mmoja katika familia yake – yaani kutoka katika familia ya Daawuud at-Twaa-iy – amehadithia kuwa alimwambia:
”Ee Abu Sulaymaan, kwani unajua ujamaa uliopo baina yetu. Ninasihi.” Macho yake yakajaa machozi kisha akasema: ”Ee ndugu kipenzi! Mchana na usiku ni vituo ambavyo watu wanakutana navyo, hatua baada ya hatua, mpaka hilo liishilie katika vituo vyao vya mwisho. Ikiwa unaweza kujizidishia katika hatua ya kila siku masurufu juu ya yale yanayokuja huko mbele, basi fanya hivo. Safari inakaribia kumalizika na jambo linakwenda haraka zaidi kuliko hivo. Kwa ajili hiyo hakikisha uko na masurufu kwa ajili ya safari yako. Fanya yale ambayo unahitaji kufanya. Kana kwamba uko katika hali iliyokushtukiza. Nijuavyo ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyeyapoteza kama mimi.” Kisha akasimama na kuniacha.
194 – al-Hasan bin Abiy Bakr ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametuzindua: Ishaaq bin Ibraahiym bin Sunayn ametuhadithia: ´Umar bin Muhammad bin Ahmad ametusomea:
Wewe uko katika upumbaaji wa matumaini
na hujui ni lini utafika wakati
Usidanganyike na uzima ambao
ni miongoni mwa magonjwa yenye aibu zaidi
Kila nafsi inayo
asubuhi inayokata matumaini
Hivyo basi, fanya kheri na ujitahidi
Kabla ya kuzuilika na matendo
195 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq ametukhabarisha: Muhammad bin Ahmad al-Baraa’ ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad al-Ash´ariy al-Madiyniy ameninakilia Mahmuud:
Jana yako ilikuwa ni shahidi wa kweli –
na hivi sasa umeraukiwa na shahidi dhidi yako
Ikiwa jana ulitenda dhambi basi fanya
leo wema ili uwe mwenye kusifiwa
Usicheleweshe hata siku moja kufanya matendo mema –
pengine kesho ikafika na wewe haupo
Ukiisimanga siku yako basi manufaa yake yanakurejelea wewe –
siku ya jana si yenye kurudi
196 – Ibn Rizq ametukhabarisha: ´Uthmaan bin Ahmad ametuzindua: Muhammad bin Ahmad bin al-Baraa’ ametuhadithia: Daawuud bin Rushayd ametuhadithia: al-Waliyd bin Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa bwana mmoja, aliyesema:
”Nilimuota Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akanambia: ”Ambaye yanalingana masiku yake mawili basi amekula khasara. Ambaye siku yake ya kesho ni ovu zaidi kuliko siku zake mbili basi amelaaniwa. Ambaye hajui mapungufu ya nafsi yake basi anapelekwa katika mapungufu na ambaye anapelekwa katika mapungufu basi kufa ni bora kwake.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 107-109
- Imechapishwa: 27/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)