42. Allaah humlinda mja Wake dhidi ya ulimwengu

190 – Abu Muusa ametuhadithia: Muhammad bin Jahdhwam ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Ja´far, kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah, kutoka kwa ´Aaswim bin ´Umar bin Qataadah, kutoka kwa Mahmuud bin Labiyd, kutoka kwa Qataadah bin an-Nu´maan, amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anapompenda mja, basi humlinda na dunia kama vile mmoja wenu anavyomkinga mtoto wake mgonjwa kutokana na maji.”[1]

191 – ´Abdul-Wahhaab bin adh-Dhwahhaak ametukhabarisha mfano wa hayo: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametukhabarisha, kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah, kutoka kwa ´Aaswim bin ´Umar bin Qataadah, kutoka kwa Mahmuud bin Labiyd, kutoka kwa Qataadah bin an-Nu´maan, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] at-Tirmidhiy (2036). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2036).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 49
  • Imechapishwa: 13/07/2025