Amesema (Ta’ala) kuhusu wale ambao hawakumtakasa Allaah kutokana na yale kasoro na mapungufu aliyojitakasa Mwenyewe ambayo hayalingani na utukufu na ukamilifu Wake (Subhaanah):
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
”Wamesema ”Mwingi wa rehema amejifanyia mwana!” Kwa hakika mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno. Zinakaribia mbingu kupasuka kwa hilo na ardhi kuraruka na milima kuporomoka na kubomoka! Kwa kule kudai kwao kuwa Mwingi wa rehema ana mwana! Wala haistahiki kwa Mwingi wa rehema kujifanyia mwana!”[1]
Hawa wamekosea inapokuja katika kumtakasa Allaah kutokana na upungufu mmoja tu; kuwa na mtoto. Yeye ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. Mola (Subhaanah) alielezea kosa lao kuwa “lenye kuchukiza mno”, mbaya na khatari sana. Ni kubwa kiasi cha kwamba mbingu, kutokana na ukubwa wake, imekaribia kupasuka vipandevipande, na ardhi, licha ya upande wake, kupasuka, na milima, licha ya nguvu na umadhubuti wake, kudidimia ndani zaidi. Yote hayo ni kwa sababu ya maneno yao yasiyo ya kidhuluma, ambayo yamebeba upotovu mkubwa inapokuja katika kuhusiana sifa moja miongoni mwa sifa za Mola (Subhaanah). Vipi basi juu ya watu wenye makosa mengi katika suala hili na wakaingia ndani ya batili aina mbalimbali?
[1] 19:88-92
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 63-64
- Imechapishwa: 04/12/2025
Amesema (Ta’ala) kuhusu wale ambao hawakumtakasa Allaah kutokana na yale kasoro na mapungufu aliyojitakasa Mwenyewe ambayo hayalingani na utukufu na ukamilifu Wake (Subhaanah):
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
”Wamesema ”Mwingi wa rehema amejifanyia mwana!” Kwa hakika mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno. Zinakaribia mbingu kupasuka kwa hilo na ardhi kuraruka na milima kuporomoka na kubomoka! Kwa kule kudai kwao kuwa Mwingi wa rehema ana mwana! Wala haistahiki kwa Mwingi wa rehema kujifanyia mwana!”[1]
Hawa wamekosea inapokuja katika kumtakasa Allaah kutokana na upungufu mmoja tu; kuwa na mtoto. Yeye ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. Mola (Subhaanah) alielezea kosa lao kuwa “lenye kuchukiza mno”, mbaya na khatari sana. Ni kubwa kiasi cha kwamba mbingu, kutokana na ukubwa wake, imekaribia kupasuka vipandevipande, na ardhi, licha ya upande wake, kupasuka, na milima, licha ya nguvu na umadhubuti wake, kudidimia ndani zaidi. Yote hayo ni kwa sababu ya maneno yao yasiyo ya kidhuluma, ambayo yamebeba upotovu mkubwa inapokuja katika kuhusiana sifa moja miongoni mwa sifa za Mola (Subhaanah). Vipi basi juu ya watu wenye makosa mengi katika suala hili na wakaingia ndani ya batili aina mbalimbali?
[1] 19:88-92
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 63-64
Imechapishwa: 04/12/2025
https://firqatunnajia.com/41-wamemnasibishia-allaah-upungufu-mmoja-tu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket