Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ama jibu la kina, kwa hakika maadui wa Allaah wana vipingamizi vingi dhidi ya dini ya Mitume, [vipingamizi] ambavyo wanawazuia kwavyo watu. Katika [vipingamizi hivyo] ni pamoja na kusema kwao:

“Sisi hatumshirikishi Allaah, bali sisi tunashuhudia ya kwamba hakuna mwenye kuumba, wala hakuna mwenye kuruzuku, wala hakuna mwenye kunufaisha wala kudhuru isipokuwa Allaah pekee asiyekuwa na mshirika, na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamiliki katika nafsi yake si manufaa wala madhara, sembuse ´Abdul-Qaadir au mwengine yeyote. Lakini mimi ni mwenye kufanya madhambi na hawa watu wema wana jaha mbele ya Allaah. Ninamuomba Allaah kwa kupitia kwao.”

Mjibu kwa yaliyotangulia, nayo ni:

“Wale ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipigana nao vita walikuwa wanakubali hayo uliyoyataja. Na walikubali ya kwamba waungu wao wa batili hawaendeshi kitu, isipokuwa tu walichokuwa wanataka ni jaha na uombezi.

MAELEZO

Jibu la kwanza lilikuwa la kijumla ambapo kumeraddiwa hoja tata zote. Vilevile kuna jibu la kina ambalo linaraddi kila utata kivyake. Mshirikina akisema: “Sisi hatumshirikishi Allaah. Tunashuhudia ya kwamba hakuna mwenye kuumba, mwenye kuruzuku, mwenye kunufaisha na kudhuru mwengine asiyekuwa Allaah pekee, hali ya kuwa hana mshirika, na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamiliki manufaa wala madhara, sembuse ´Abdul-Qaadir – yaani Ibn Muusa al-Jiylaaniy. Alikuwa ni mtu mkubwa mwenye kuipa kisogo dunia na Suufiyyah. Alizaliwa 471 Jiylaan na kufariki 561 Baghdaad na alikuwa akifuata madhehebu ya Hanbaliy – na hii ndio Tawhiyd!”, unatakiwa kutambua kuwa hii ni hoja tata anaouvisha uongo kwao. Hata hivyo ni utata dhaifu na usiokuwa na maana yoyote.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Lakini mimi ni mwenye kufanya madhambi… “

Haya ni mwendelezo wa maneno ya mpinzani. Mjibu kwa kumwambia aliyosema ndio yaleyale waliyosema washirikina. Pamoja na hivyo, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawapiga vita na akahalalisha damu, wanawake na mali zao kuchukuliwa. Aina hii ya Tawhiyd haikuwanufaisha chochote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 60
  • Imechapishwa: 11/11/2023