Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

69 – Hatusemi kuwa dhambi haiathiri imani kwa yule mwenye kuitenda.

MAELEZO

Hata hivyo Murji-ah wanaona kuwa dhambi haziathiri imani. ´Aqiydah yao inapelekea katika kukadhibisha Aayah za makemeo na Hadiyth zilizopokelewa kuhusu watenda madhambi wa ummah huu na kwamba wako miongoni mwao watakaoingia Motoni kisha baadaye watolewe kwa uombezi au sababu nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 63
  • Imechapishwa: 01/10/2024