188 – Ibn Kaasib ametuhadithia: Ibn Abiy Fudayk ametukhabarisha, kutoka kwa Kathiyr bin Zayd, kutoka kwa al-Muttwalib, kutoka kwa bwana mmoja aliyemsikia Ibn ´Umar akisema:

“Nilimkumbuka Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Alisimama mahali ninaposimama sasa, akalitazama jua katika umbo lake la sasa na kusema: “Enyi watu! Hakika hakuna kilichobaki katika dunia yenu, kati ya kile kilichopita, isipokuwa ni kama kile kilichobaki katika siku yenu hii kati ya kile kilichopita ndani yake.”[1]

189 – Muhammad bin Ismaa´iyl ametukhabarisha: ´Iysaa bin Ibraahiym al-Baswriy ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Muslim ametukhabarisha: Matwar al-Warraaq ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudhriy, ambaye ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alizungumza nasi mpaka ukabaki tu mwanga mwekundu kwenye majani ya mitende. Akasema: ”Hakika hakuna kilichobaki katika dunia yenu, kati ya kile kilichopita, isipokuwa ni kama kile kilichobaki katika siku yenu hii.”[2]

[1] Ahmad (2/133) ambayo cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir.

[2] at-Tirmidhiy (2191), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 13/07/2025