Imekuja katika Hadiyth nyingine ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah (Ta´ala) atasema: “Ee Aadam!” Atajibu: “Ninaitikia wito Wako na nakuomba unifanye ni mwenye furaha na mafanikio.” Kisha Ataita kwa sauti: “Hakika Allaah anakuamrisha utoe moja katika kizazi chako Motoni.”
Hapa kunathibitishiwa Allaah sauti na kwamba Yeye (Subhaanah) anayo sauti yenye kusikika. Sauti hiyo wanaisikia Malaika, Muusa (´alayhis-Salaam) aliisikia na pia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliisikia katika safari ya usiku aliyopandishwa mbinguni. Amesema:
“Hakika Allaah anakuamrisha utoe moja katika kizazi chako Motoni.”
Imekuja katika Hadiyth nyingine:
Imekuja katika Hadiyth nyingine ya kwamba miongoni mwa watu 1000 basi kuna 999 watakaoingia Motoni na kwamba mtu mmoja pekee ndiye ataokoka. Hii inaonyesha ni khatari kubwa. Kwa ajili hii ndio maana (Jalla wa ´Alaa) akasema:
وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ
“Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima.” (12:103)
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
“Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah.” (06:116)
وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ
“Hakika Ibliys alisadikisha dhana yake juu yao. Wakamfuata [wote] – isipokuwa kundi katika waumini wa kweli.” (34:20)
Pindi Maswahabah waliposikia kuhusu jambo hili ya kwamba katika watu 1000 ataokoka 1 tu, jambo hili lilikuwa zito kwao. Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia mwishoni mwa Hadiyth:
“Msikhofu! Hawa 999 ni katika Ya´juu na Ma´juuj. Miongoni mwenu kuna mmoja tu katika ummah wa Muhammad.”
Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa wengi wataoingia Motoni wanatokana na Ya´juuj na Ma´juuj. Hawa ni watu waovu kabisa ambao watajitokeza katika zama za mwisho.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 58-59
- Imechapishwa: 23/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket