119 – Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapomaliza kuswali anaomba msamaha mara tatu na akisema:

اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلَامُ، وَمِنْكَ السَّلَامُ ، تَبَارَكْتَ ذَا الْجَلَالِ وَالإِكْرَامِ

”Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam na amani inatoka Kwako na umetukuka, Mwenye utukufu na ukarimu.”

al-Waliyd amesema: “Nikamuuliza al-Awzaa´iy ni vipi kuomba msamaha?” Akasema: “Aseme:

أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ ، أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ

“Namuomba Allaah msamaha, namuomba Allaah msamaha.”[1]

Ameipokea Muslim.

120 – ´Aiashah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotoa salamu haketi chini isipokuwa kwa kiwango cha kusema:

اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلَامُ، وَمِنْكَ السَّلَامُ ، تَبَارَكْتَ ذَا الْجَلَالِ وَالإِكْرَامِ

”Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam na amani inatoka Kwako na umetukuka, Mwenye utukufu na ukarimu.”

Imekuja katika upokezi wa Ibn Numayr:

يَا ذَا الْجَلَالِ وَالإِكْرَامِ

“Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”[2]

Ameipokea Muslim.

121 – al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema mwishoni mwa swalah zote za faradhi:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، اللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.  Ee Allaah! Hakuna awezaye kuzuia ulichokitoa na wala kutoa ulichokizuia na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.”[3]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

122 – Abu az-Zubayr amesimulia: “Ibn-uz-Zubayr alikuwa akisema mwishoni mwa kila swalah wakati anapotoa salamu:

لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.  Hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, wala hatumwabudu mwengine isipokuwa Yeye, ni Zake neema, fadhilah ni Zake na ni Zake sifa zote nzuri, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kumtakasia Yeye dini, ijapokuwa watachukia makafiri.”

Amesema: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyasema mwishoni mwa kila swalah.”[4]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hizi kuna ubainifu wa Adhkaar ambazo zinasemwa na muislamu baada ya kumaliza kuswali. Adhkaar hizi muislamu anazisema punde tu baada ya kumaliza swalah yake. Atasema:

أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ, أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ, أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ

“Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha. Namuomba Allaah msamaha.”

Kisha aseme:

اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلَامُ، وَمِنْكَ السَّلَامُ ، تَبَارَكْتَ ذَا الْجَلَالِ وَالإِكْرَامِ

”Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam na amani inatoka Kwako na umetukuka, Mwenye utukufu na ukarimu.”

Halafu kama ni imamu anatakiwa kuwageukia waswaliji:

لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير، لا حول ولا قوة إلا بالله، لا إله إلا الله ولا نعبد إلا إياه، له النعمة وله الفضل، وله الثناء الحسن، لا إله إلا الله مخلصين له الدين ولو كره الكافرون، اللهم لا مانع لما أعطيت ولا معطي لما منعت، ولا ينفع ذا الجد منك الجد

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.  Hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, wala hatumwabudu mwengine isipokuwa Yeye, ni Zake neema, fadhilah ni Zake na ni Zake sifa zote nzuri, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kumtakasia Yeye dini, ijapokuwa watachukia makafiri. Ee Allaah! Hakuna awezaye kuzuia ulichokitoa na wala kutoa ulichokizuia na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.”

[1] Muslim (591).

[2] Muslim (592).

[3] al-Bukhaariy (844) na Muslim (593).

[4] Muslim (594).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 115-116
  • Imechapishwa: 09/11/2025