Amesema (Ta’ala) kuhusu wale ambao wanatilia shaka sifa moja tu:
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ فَإِن يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم مِّنَ الْمُعْتَبِينَ
”Hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu wala macho yenu wala ngozi zenu, lakini mlifikiria kuwa Allaah hajui mengi katika yale mnayoyatenda. Na hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Mola wenu ndiyo imekuangamizeni na mmekuwa katika waliokhasirika. Basi wakivuta subira, lakini moto ndio makazi yao tu! Wakiomba wapewe nafasi tena ya kufanya utiifu wa kumridhisha Allaah, basi wao si wenye kuridhishwa na kupewa.”[1]
Watu hawa wametilia shaka ujuzi wa Allaah. Wakafikiria kwamba Allaah hajui mengi katika wanayoyafanya. Kwa sababu ya dhana hii mbaya na imani mbovu wakaingia ndani ya batili na upotofu. Vipi basi kwa yule ambaye anatilia shaka sifa Zake zote au angalau nyingi kati ya hizo? Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anh) amesema kuhusiana na Aayah hizo zilizotangulia hapo juu:
“Watu wawili kutokana na Quraysh na shemeji yao kutoka Thaqiyf, au ilikuwa watu wawili kutoka Thaqiyf na shemeji yao kutokana na Quraysh, walikuwa kwenye nyumba. Mmoja wao akasema: ”Je, mnadhani kuwa Allaah anasikia mazungumzo yetu?” Mmoja wao akasema: “Anasikia baadhi yake.” Mwingine akasema: ”Ikiwa anasikia baadhi yake basi Anayasikia yote.” Ndipo kukateremshwa:
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ
”Hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu wala macho yenu wala ngozi zenu, lakini mlifikiria kuwa Allaah hajui mengi katika yale mnayoyatenda.”
Ameipokea al-Bukhaariy, ambaye tamko ni lake, na Muslim. Imekuja kwa Muslim:
“Watu watatu walikuwa wamekusanyika kwenye Nyumba, wawili wanatokana na Quraysh na mwingine anatokana na Thaqiyf, au kinyume chake. Walikuwa wenye akili finyu na wanene. Mmoja wao akasema: ”Je, mnadhani kuwa Allaah anasikia tunayoyasema?” Mmoja wao akasema: “Anasikia tunaposema kwa sauti ya juu na Hasikii tunaposema kimyakimya.” Mwingine akasema: “Ikiwa anasikia tunayosema kwa sauti ya juu, pia Anasikia tunaposema kimyakimya.” Ndipo Allaah (‘Azza wa Jall) akateremsha:

[1] 41:22-24
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 62-63
- Imechapishwa: 04/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 62-63
Imechapishwa: 04/12/2025
https://firqatunnajia.com/40-walitilia-shaka-sifa-moja-tu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket