187 – al-Hulwaaniy ametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametukhabarisha: ´Abdul-Waahid bin Zayd ametukhabarisha: Aslam al-Kuufiy ametukhabarisha, kutoka kwa Murrah at-Twayyib, kutoka kwa Zayd bin Arqam, kutoka kwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alizuia kitu na huku akisema: ”Niondokee mbali! Niondokee mbali!” Hata hivyo sikumuona yeyote pamoja naye, ndipo nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nilikuona ukizuia kitu lakini sikumuona mtu yeyote pamoja nawe.” Akasema: “Ilikuwa ni dunia ambayo imeonyeshwa kwangu na vilivyomo ndani yake. Nikasema: ”Niondokee mbali!” Ikaondoka na kusema: “Naapa kwa Allaah! Ikiwa umesalimika nami basi hawatosalimika nami watakaokuja baada yako.”[1]
[1] Dhaifu mno kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (4878).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 48
- Imechapishwa: 13/07/2025
187 – al-Hulwaaniy ametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametukhabarisha: ´Abdul-Waahid bin Zayd ametukhabarisha: Aslam al-Kuufiy ametukhabarisha, kutoka kwa Murrah at-Twayyib, kutoka kwa Zayd bin Arqam, kutoka kwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alizuia kitu na huku akisema: ”Niondokee mbali! Niondokee mbali!” Hata hivyo sikumuona yeyote pamoja naye, ndipo nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nilikuona ukizuia kitu lakini sikumuona mtu yeyote pamoja nawe.” Akasema: “Ilikuwa ni dunia ambayo imeonyeshwa kwangu na vilivyomo ndani yake. Nikasema: ”Niondokee mbali!” Ikaondoka na kusema: “Naapa kwa Allaah! Ikiwa umesalimika nami basi hawatosalimika nami watakaokuja baada yako.”[1]
[1] Dhaifu mno kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “adh-Dhwa´iyfah” (4878).
Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 48
Imechapishwa: 13/07/2025
https://firqatunnajia.com/40-ummah-hautosalimishwa-na-dunia/