Madhehebu ya ash-Shaafi´iyyah:
Imaam at-Tirmidhiy amesema:
”Mlango wa kupaka juu ya soksi na viatu
Hannaad na Mahmuud bin Ghaylaan wametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Qays, kutoka kwa Huzayl bin Shurahbiyl, kutoka kwa al-Mughiyrah bin Shu´bah ambaye amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa soksi (الجوربين) na viatu.”
Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
Nayo ni maoni ya zaidi ya mmoja miongoni mwa wanazuoni, na ndivyo wanavyosema Sufyaan ath-Thawriy, Ibn-ul-Mubaarak, ash-Shaafi´iy, Ahmad na Ishaaq. Wamesema:
”Hupakwa juu ya soksi hata kama hazina soli ya ngozi, ikiwa ni nzito.”[1]
Inajulikana ya kwamba Imaam at-Tirmidhiy amepokea kutoka kwa wanafunzi wa Imaam ash-Shaafi´iy. Amesema:
”Kuhusiana na maoni ya ash-Shaafi´iy, mengi katika hayo ni yake aliyonisimulia al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy kutoka kwa ash-Shaafi´iy. Yale yanayohusiana wudhuu´ na swalah Abul-Waliyd al-Makkiy ndiye ametuhadithia kutoka kwa ash-Shaafi´iy. Miongoni mwa hayo ametuhadithia pia Abu Ismaa´iyl akasema: Yuusuf bin Yahyaa al-Qurashiy al-Buwaytiy ametuhadithia, kutoka kwa ash-Shaafi´iy. Mambo mengine yametajwa kutoka kwa ar-Raabiy´, kutoka kwa ash-Shaafi´iy. ar-Rabiy´ ameturuhusu kufanya hivo na akatuandikia juu ya suala hilo.”[2]
Imaam ash-Shiyraaziy amesema katika ”al-Muhadhdhab”:
”Akivaa soksi basi inajuzu kupangusa juu yake kwa sharti mbili: Ya kwanza ziwe nzito zisizopenya kuonyesha na ya pili ziwe na soli.”
an-Nawawiy amesema akiyatolea maelezo:
”Hivi ndivyo walivyokata kauli kundi miongoni mwao kama vile Shaykh Abu Haamid, al-Muhaamiliy, Ibn-us-Sabbaagh na wengineo. al-Muzaniy amenukuu kwamba hakupanguswi juu ya soksi isipokuwa ziwe zimefunikwa ngozi katika sehemu ya miguu… Lililo sahihi, bali lililo sawa, ni yale yaliyotajwa na Qaadhwiy Abut-Twayyib al-Qaffaal na kikosi katika wahakiki, nayo ni kwamba ikiwa inawezekana kutembea nazo basi inajuzu kupangusa juu yake, la sivyo hapana.”
[1] al-Jaamiy´ (99).
[2] al-´Ilal, uk. 484.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 65-66
- Imechapishwa: 15/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 65-66
Imechapishwa: 15/04/2026
https://firqatunnajia.com/40-madhehebu-ya-ash-shaafiiyyah-kuhusu-kupangusa-juu-ya-soksi/