Madhehebu ya Maalikiyyah:
Imaam Ibn-ul-Qaasim amesema katika ”al-Mudawwanah”:
”Maalik alikuwa akisema kuhusu soksi zinazokuwa miguuni na chini yake kuna ngozi iliyoshonwa na juu yake ngozi iliyoshonwa kwamba zinapakwa juu yake. Kisha akarudi akasema kuwa hazipanguswi juu yake.”
Ibn-ul-Qaasim amesema:
”Maoni yake ya kwanza ndiyo yanayopendeza zaidi kwangu ikiwa juu yake kuna ngozi, kama nilivyokueleza.”
Ibn Yuunus amesema:
”Nayo – yaani kauli ya kwanza ya Maalik – ndiyo sahihi, kwa sababu ikiwa juu yake kuna ngozi iliyoshonwa inayofika vifundoni basi hii ni kama soksi za ngozi.”
Ibn-ul-Qaasim kupendezwa na maoni ya kwanza ya Imaam Maalik na maneno ya Ibn Yuunus aliposema wazi kwamba maoni ya kwanza ndio sahihi ni dalili kubwa kwamba wanafunzi wa maimamu walikuwa wakijiepusha na kufuata kipofu tu na hawakutegemea isipokuwa dalili na hilo likawa kwa hakika ni madhehebu yao. Hivyo ndivyo ilivyokuwa hali ya wanafunzi wawili wa Abu Haniyfah pamoja naye. Pia hivyo ndivyo walivyokuwa wanafunzi wa ash-Shaafi´iy, kwani al-Muzaniy mara nyingi alijitenga na maoni ya mwalimu wake ash-Shaafi´iy. an-Nawawiy amenukuu katika ”al-Majmuu´” kutoka kwa Imaam al-Haramayn kwamba al-Muzaniy anapojitenga kwa maoni basi yeye ndiye mwenye kutangulizwa katika madhehebu. Wengi katika wanafunzi wa ash-Shaafi´iy wamechagua baadhi ya masuala yake aliyoyaacha na wakatoa fatwa kwayo baada yake. Imaam al-Haramayn amesema:
”Maoni yaliyorejewa si madhehebu ya aliyejirejea; basi inapojulikana hali ya kauli ya zamani na tukawakuta wanafunzi wetu wametoa fatwa katika masuala haya kwa kauli ya zamani, basi tunachukua hilo kwamba ijtihadi yao imewafikisha kwenye kauli ya zamani kwa uwazi wa dalili yake na wao ni Mujtahiduun.”
Basi zingatia maneno yake ”na wao ni Mujtahuun” utaona kosa la yale wanayosema baadhi kwamba wao ni Mujtahiduun ndani ya madhehebu tu si Mujtahiduun kwa ujumla. Wao si Mujtahiduun kwa ujumla. Si kila Mujtahid ana wafuasi na madhehebu iliyoandikwa. Uhakika wa mambo ni kwamba hata kama kauli itatolewa juu ya misingi ya imamu wa madhehebu, haitakuwa madhehebu yake. Imaam an-Nawawiy amesema:
”Tayari yamekwishatangulia tofauti yao kama aliyetoka atanasibishwa kwa ash-Shaafi´iy. Llilo sahihi zaidi ni kwamba hatonasibishwa.”
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 63-65
- Imechapishwa: 15/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 63-65
Imechapishwa: 15/04/2026
https://firqatunnajia.com/39-maoni-mashuhuri-ya-maimamu-kuhusu-kupangusa-juu-ya-soksi/