24 – Kutolazimiana na Hijaab inayokubalika katika Shari´ah

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni kutolazimiana na Hijaab inayokubalika katika Shari´ah. Baadhi ya wasichana – Allaah awaongoze – huvaa mavazi yanayofika kwenye vifundo vya miguu tu, jambo ambalo si la sawa. Wengine huvaa Hijaab zenye mapambo ya kuvutia, zinazofanya macho kumgeukia, au wanavaa mavazi yenye harufu nzuri, yaliyobana yanayouchora mwili, mafupi au yaliyopasuliwa kando. Haya yote hayafai kwa sababu ni katika kuonyesha mapambo.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 34
  • Imechapishwa: 22/03/2026