Wakati mtu anaponyenyekeza viungo vyake vya mwili pasi na moyo wake, unakuwa ni unyenyekevu wa unafiki. Huo ndio unyenyekevu ambao Salaf walikuwa wakijilinda nao. Mmoja wao ambaye amesema:

”Jilinde kwa Allaah kutokana na unyenyekevu wa unafiki.” Wakasema: ”Ni upi unyenyekevu wa unafiki?” Akasema: ”Ni kuona viungo vya mwili vimenyenyekea lakini moyo haukunyenyekea.”

Siku moja ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alimuona kijana mmoja ameinamisha kichwa chake akamwambia:

”Ee wewe! Inua kichwa chako! Unyenyekevu hauzidi yale yaliyomo moyoni.”

Yule anayeonyesha unyenyekevu zaidi ya yaliyomo ndani ya moyo ni unafiki tu juu ya mwingine. Msingi wa unyenyekevu unaopatikana ndani ya moyo unatokana na utambuzi wa Allaah, utukufu Wake, ukuu na ukamilifu Wake. Kadri mtu anavyomjua zaidi Allaah, ndivyo anavyojinyenyekeza zaidi Kwake.

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 24/11/2025