Ilipokuwa suala hili lina hadhi na umuhimu huu, basi nikapenda kuwasilisha utafiti wa moja ya masimulizi kutoka kwa Salaf (Rahimahumu Allaah), ambayo yanathibitisha upwekeshaji na kuwaraddi watu wa Bid´ah na wenye kufuata matamanio, ili kudhihirisha faida, matunda na manufaa ya kutilia umuhimu maneno ya Salaf. Kwa hivyo nikawa na bidii kuandaa masimulizi haya yanayotambulika kutoka kwa Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) pale ambapo alimjilia bwana mmoja na kumwambia:
”Ee Abu ´Abdillaah!
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
Amelingana juu vipi?”
Akachukulia vibaya, ndipo akaanza kutokwa na jasho na huku watu wanasubiri wasikie atachosema. Kisha akajivuta na kusema: ”Kulingana juu si kitu kisichojulikana. Namna si kitu kisichofahamika. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo. Nachelea ukawa mpotevu.”
Akaamrisha muulizaji akatolewe katika kikao chake. Masimulizi haya ni yenye hadhi na faida kubwa.
Motisha muhimu zilizonifanya kufanya utafiti wa masimulizi haya ni pamoja na:
1 – Watu wameyapokea kwa kuyakubali. Hakuna yeyote katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambaye ameyapinga, kama alivosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)[2]. Bali wanazuoni wameyatilia umuhimu, wakayatilia bidii na kuyaona ni mazuri.
2 – Jibu la swali hili ni mojawapo ya majibu mazuri na ya kina ambayo yametolewa juu ya mada hii. Kwa upande mmoja limetupilia mbali kule kufanya namna, kwa upande mwingine kunathibitisha kulingana juu kunakotambulika kwa mujibu wa lugha vile inavyolingana na Allaah (‘Azza wa Jall)[3].
3 – Maneno yake haya sio maalum juu ya Kulingana juu, bali yanatumika juu ya sifa nyenginezo zote.
4 – Wazushi, katika zama zote, wanajaribu kubadilisha maana na kukengeusha makusudio yake kwa njia za kujikakama na mbinu mbalimbali.
5 – Mmoja katika wajinga wa leo amejaribu kuhoji kuthibiti kwake na akaponda cheni zake za wapokezi.
6 – Zinduo ya jinsi baadhi ya wafuasi wa maimamu katika mambo ya mataga hawakuwafikishwa kupatiliza ´Aqiydah ya maimamu wao. Kwa ajili hiyo unaweza kuwaona baadhi ya wale ambao ni washupavu wa madhehebu ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) katika masuala ya matawi wanavyokwenda kinyume naye katika masuala ya ´Aqiydah. Kwa msemo mwingine wanatofautiana naye katika misingi ya ´Aqiydah kwa sababu ya kuenea kwa matamanio na kuenea kwa Bid´ah.
Kwa ajili hiyo nimefanya utafiti huu kuitwa “al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa'”. Kuhusu madhumuni ya utafiti huu ni kuyapa masimulizi haya hadhi yake stahiki na kunyofoa humo mazingatio na kanuni za kielimu na kuraddi upotoshaji wa wapinzani na hoja tata za wapotoshaji.
[1] 20:5
[2] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (5/520).
[3] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (5/520).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 9-10
- Imechapishwa: 26/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 9-10
Imechapishwa: 26/11/2025
https://firqatunnajia.com/4-ndio-maana-ikawa-muhimu-kusoma-jawabu-la-maalik-kuhusu-kulingana-juu/