´Aliy al-Halabiy ni katika watu wabaya zaidi wanaoshuhudia batili. Anashuhudia kwa watu wapotevu na wenye misingi ilioharibika na mifumo batili ya kwamba ni Salafiyyuuun, amesimama upande wao na kutumia misingi na mifumo yao. Miongoni mwa watu hawa ni:
3- Abul-Hasan al-Miswriy al-Ma´ribiy al-Ikhwaaniy
Mwanzoni alikuwa akionyesha Salafiyyah. Pale ambapo wanachuoni wakubwa wa Ahl-us-Sunnah walifariki kama ´Allaamah Ibn Baaz, ´Allaamah al-Albaaniy, ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn na ´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy akawavamia Salafiyyuun na kuwatukana vibaya sana. Akawatuhumu kuwa ni wajinga, watu wafupi na matusi mengine. Akajitenga mbali na wao na kupambana nao kiasi cha kwamba hatimae akawaita Maswahabah kuwa ni “povu” na “wadogo chini ya miguu ya wengine”.
Akaunda misingi ili kupiga vita mfumo wa Salaf na Salafiyyuun kwa mfano “mfumo mpana wenye kuingia ndani yake Ahl-us-Sunnah na Ummah wote”, “tunasahihisha na hatubomoi” na misingi mingine mingi.
Wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wamemnasihi kurejea katika haki, lakini akakataa. Baada ya hapo akawapuuza wanachuoni wa Yemen na Saudi Arabia. Akaendelea na fitina zake na upotevu wake mpaka akaanza kuwatetea wapotevu ambao wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah, waarabu na wasiokuwa waarabu, wamekubaliana ya kwamba ni wapotevu kwa mfano wa al-Ikhwaan al-Muslimuun ambao wako na Suufiyyah walopetuka mipaka, Raafidhwah, Khawaarij na manaswara, wanashirikiana na wakomunisti na wanasekula na kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa njia iliyo mbaya sana.
Wengine katika hawa ni Jamaa´at-ut-Tabliygh ambao wanatoa kiapo cha usikivu na utiifu [bay´ah] kuwapa mapote mane ya Suufiyyah na imejengwa juu ya Shirki, imani ya kwamba Allaah Yuko katika kila kitu [Huluul] na imani ya kwamba kila kitu ni Allaah [Wahdat-ul-Wujuud].
Abul-Hasan anasema kuwa mapote haya mawili ni katika Ahl-us-Sunnah na kuonelea kuwa wanasekula, wana-ujamaa (socialists) na kundi la Ba´th ni waislamu. Hakumkufurishi yeyote katika wao, si viongozi wao wala wafuasi wao.
Ameandika kitabu kinachoitwa “ad-Difaa´ ´an Ahl-il-Ittibaa´” ambapo ndani yake amewatetea al-Ikhwaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliygh na viongozi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun wanaolingania katika umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini. Kwenye utetezi huo amefanya udanganyifu wa kielimu ambao unaweza kufanywa tu na mtu sampuli yake. Ukiongeza juu ya hilo ni kwamba amekuwa mpotevu zaidi na zaidi.
al-Halabiy na wafuasi wake wamesimama upande wake na kuonelea kuwa ni Salafiy na ni katika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah.
Je, ushuhudiaji wa al-Halabiy ya kwamba al-Ma´ribiy ni Salafiy si ni mfano wa ushuhudiaji wa uongo ulio mbaya sana na uendaji kinyume ulio mkubwa wa mfumo wa Salaf? Je, kitendo hichi hakibomoi msingi wa kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah? Je, si ni mfano wa mgongano ulio mkubwa kudai Salafiyyah kisha baadaye mtu akawa na wapinzani wake? Haya majanga makubwa yamefanywa na al-Halabiy na kundi lake na wamejengwa juu ya matamanio.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/4-al-halabiy-na-al-maribiy/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)