39. Unawanasihi vipi wanafunzi wanaoghushi mtihani katika Ramadhaan?

Swali 39: Tunataka uwape nasaha vijana wanaoghushi mtihani katika Ramadhaan?

Jibu: Wanafunzi wamenishinda na hawasikilizi maneno yangu. Wakati nilipokuwa nikiwachunga katika mtihani nilikuwa nawakumbusha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kujipamba kwa kitu asichokuwa nacho ni kama mtu aliyevaa nguo mbili za uongo.”[1]

Ni juu yako kutosheka na elimu uliyopewa na Allaah. Inakutosha kutatua matatizo.

[1] al-Bukhaariy (5219) na Muslim (2129).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 57