3 – Amesema kuwa ni wajibu kuliamini hilo. Akimaanisha kulingana juu ambako Mola (Subhaanah) amejieleza Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake na akaelezwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya Sunnah zake. Msimamo huohuo ndio unapaswa kuchukuliwa juu ya sifa zote zilizotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah; ni wajibu kuziamini na kuzipitisha vile zilivyokuja pasi na kuzikanusha, kuzipotosha, kuzifanyia namna, kuzilinganisha na mfano wa hayo. Kwa ajili hiyo mara nyingi Allaah anawahimiza na kuwasisitiza waja Wake kujifunza majina na sifa za Mola, kuziamini na kuzitambua utambuzi sahihi na uliosalimika. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلِلّهِ الأَسْمَاء الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا وَذَرُواْ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَآئِهِ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ
”Allaah ana majina mazuri mno; hivyo basi muombeni kwayo na waacheni wale wanaopotoa katika majina Yake. Watalipwa yale waliokuwa wakifanya.”[1]
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ
“Sema: “Muiteni Allaah au muiteni ar-Rahmaan”, vovyote mtakavyomwita basi [tambua kuwa] Yeye ana majina mazuri kabisa.”[2]
هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
”Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, mjuzi wa yaliyofichikana na ya dhahiri, Yeye ni Mwenye kurehemu. Yeye ni Allaah, ambaye hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, mfalme, mtakatifu, Mwenye kusalimisha na kusalimika, Mwenye kusadikisha ahadi na kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye nguvu zisizoshindwa, Jabari, Mwenye ukubwa na utukufu – Utakasifu ni wa Allaah kutokamana na ambayo wanamshirikisha. Yeye ni Allaah, muumbaji, mwanzishi viumbe, muundaji sura – ana majina mazuri mno. Kinamtukuza kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi Naye ni Mwenye nguvu zisizoshindwa, Mwenye hekima.”[3]
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا
”Allaah ndiye ambaye ameziumba mbingu saba na katika ardhi mfano wa hizo, inateremka amri kati yao ili mjue kwamba Allaah juu ya jambo ni Muweza na kwamba Allaah amekizunguka kila kitu kwa Ujuzi.”[4]
فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
”Lakini mkiteleza baada ya kukujieni ubainifu, basi tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mwenye nguvu Asiyeshindika, Mwenye hekima.”[5]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ
”Mcheni Allaah na tambueni ya kwamba Allaah ni Mjuzi wa kila jambo.”[6]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
”Tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mwenye kuona yale myatendayo.”[7]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ
”Tambua ya kwamba Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mvumilivu.”[8]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
”… na tambueni kwamba Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.”[9]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ
”Tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[10]
اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Jueni kuwa Allaah ni Mkali wa kuakibu na kwamba Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.”[11]
وَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَوْلَاكُمْ ۚ نِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ
”… na wakikengeuka, basi tambueni ya kwamba Allaah ni Mlinzi wenu – Mlinzi mzuri aliyoje na mnusuruji mzuri aliyoje!”[12]
وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ
”… na mcheni Allaah na tambueni kwamba Allaah yupamoja na wamchao.”[13]
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ
”Tambueni kwamba Allaah anajua yaliyomo katika nafsi zenu, basi jihadharini Naye!”[14]
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ
“Basi jua kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”[15]
Kuna Aayah nyingi mfano wa hizo. Aayah hizi na zinazofanana na hizi zinasisitiza namna ilivyo muhimu kuamini majina mazuri na sifa kuu za Mola (Tabaarak wa Ta´ala) na kwamba jambo hilo ni miongoni mwa misingi iliyoimarishwa ya imani na nguzo kubwa kabisa ambazo imani haipatikani isipokuwa kwavyo. Kwa hivyo yule mwenye kuzikanusha, au akapinga kitu katika hizo, sio muumini. Allaah (Ta´ala) juu ya wale wenye kukufuru jina la Mwingi wa rehema (الرَّحْمَن):
وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ
“… nao wanamkufuru Mwingi wa rehema.”[16]
Kusemwe nini juu ya ambaye anapinga majina au sifa Zake zote?
[1] 7:180
[2] 17:110
[3] 59:22-24
[4] 65:12
[5] 2:209
[6] 2:231
[7] 2:233
[8] 2:235
[9] 2:244
[10] 2:267
[11] 5:98
[12] 8:40
[13] 2:194
[14] 2:235
[15] 47:19
[16] 13:30
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 60-62
- Imechapishwa: 04/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 60-62
Imechapishwa: 04/12/2025
https://firqatunnajia.com/39-ni-wajibu-kuamini-kulingana-juu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket