Swali: Baadhi ya watu wanapofiwa na jamaa ndani au nje ya Madiynah basi wanafanya bidii azikwe sehemu ya mbele ya Baqiy´. Pengine wanaona kuwa kuna fadhilah kuzikwa sehemu ya mbele kuliko sehemu ya nyuma. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Ikiwa maiti amekufa karibu na Madiynah basi kumzika huko ndio bora na vyema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ee Allaah! Wasamehe waliozikwa kwenye Baqiy´ yenye miiba.”[1]
Hata hvyo mtu asipelekwe huko kama amekufa sehemu ya mbali kutokea hapo.
Kuhusiana na kupendelea kwao kuzikwa sehemu ya mbele ya Baqiy´ kwa kudhani kuwa ndio bora, ni jambo halina msingi. Sehemu yote ya makaburi yanalingana.
[1] Muslim (974).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/446)
- Imechapishwa: 30/05/2026
Swali: Baadhi ya watu wanapofiwa na jamaa ndani au nje ya Madiynah basi wanafanya bidii azikwe sehemu ya mbele ya Baqiy´. Pengine wanaona kuwa kuna fadhilah kuzikwa sehemu ya mbele kuliko sehemu ya nyuma. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Ikiwa maiti amekufa karibu na Madiynah basi kumzika huko ndio bora na vyema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ee Allaah! Wasamehe waliozikwa kwenye Baqiy´ yenye miiba.”[1]
Hata hvyo mtu asipelekwe huko kama amekufa sehemu ya mbali kutokea hapo.
Kuhusiana na kupendelea kwao kuzikwa sehemu ya mbele ya Baqiy´ kwa kudhani kuwa ndio bora, ni jambo halina msingi. Sehemu yote ya makaburi yanalingana.
[1] Muslim (974).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/446)
Imechapishwa: 30/05/2026
https://firqatunnajia.com/383-ni-ipi-hukumu-ya-kuzikwa-baqiy/