Hiyo kama tulivyosema ni mifugo inayolishwa malishoni. Nayo ni aina tatu:
1 – Ngamia. Hakuna zakaah ndani yake mpaka wafikie watano. Katika hali hiyo inawajibika kondoo mmoja. Wakifikia kumi, kondoo wawili. Wakifikia kumi na tano, kondoo watatu. Wakifikia ishirini, kondoo wanne. Hadi ishirini na tano, hapo kunawajibika kutoa ngamia wa kike mwenye mwaka mmoja. Ikiwa hana huyo, basi atawajibika kutoa ngamia wa kiume mwenye miaka miwili.
Wakifikia thelathini na sita, inawajibika kutoa ngamia wa kike aliyekamilisha miaka miwili na kuingia mwaka wa tatu. Wakifikia arobaini na sita, inawajibika kutoa ngamia wa kike aliyekamilisha miaka mitatu na kuingia mwaka wa nne. Wakifikia sitini na moja, inawajibika kutoa ngamia wa kike aliyekamilisha miaka minne na kuingia mwaka wa tano. Wakifikia sabini na sita, inawajibika kutoa ngamia jike mwenye miaka miwili. Wakifikia tisini na moja, inawajibika kutoa ngamia jike mwenye miaka mitatu. Wakifikia mia moja na ishirini, hivyo ndivyo hukumu yake ilivyo. Wakizidi mmoja, basi inawajibika kutoa ngamia jike watatu wenye miaka miwili.
Kisha katika kila ngamia khamsini inawajibika kutoa ngamia jike mmoja mwenye miaka mitatu. Katika kila ngamia arobaini inawajibika kutoa ngamia jike mmoja mwenye miaka miwili, mpaka wafikie ngamia mia mbili. Hapo hukusanyika viwango viwili vya zakaah. Akipenda, atatoa ngamia majike wanne wenye miaka mitatu, na akipenda atatoa ngamia majike watano wenye miaka miwili.
Yule ambaye amewajibikiwa kutoa mnyama mwenye umri fulani lakini hakumpata, atatoa aliye chini ya umri huo pamoja na kondoo wawili au dirhamu ishirini, na akitaka, atatoa aliye juu ya umri huo na achukue kondoo wawili au dirhamu ishirini.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 35
- Imechapishwa: 25/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 35
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/38-zakaah-ya-ngamia/